1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Milipuko miwili na ufyatulianaji wa risasi wautikisa mji wa Mogadishu

Milipuko miwili na mapigano yameutikisa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu usiku wa kuamkia leo. Walioshuhudia wanasema maiti za watu wawili zilizokuwa na alama za risasi zimepatikana mapema leo karibu na kambi ya jeshi la Ethiopia kaskazini wa Mogadishu.

Maafisa wa serikali ya mpito ya Somalia wamekataa kusema lolote kuhusu milipuko hiyo na ufyatulianaji wa risasi wa usiku kucha lakini kwa mujibu ya walioshuhudia wanasema mlipuko mmoja ulisababishwa na mwanamgambo wa kiislamu wakati alipovurumisha bomu katika kituo kimoja cha polisi katika wilaya ya Huriwaa kaskazini mwa Mogadishu. Hakuna afisa yeyote wa polisi aliyejeruhiwa katika shambulio hilo. ´

Mlipuko wa pili umetokea karibu na kambi ya jeshi la Ethiopia. Ufyatulianaji wa risasai uliendelea kwa muda mrefu lakini haiubainaika wazi ni makundi gani yaliyokuwa yakipigana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com