1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mogadishu. Mapigano yaendelea.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6w

Mapigano zaidi yameripotiwa kutokea katika mji wa Mogadishu nchini Somalia, wakati majeshi ya Ethiopia yakiunga mkono serikali ya mpito ya nchi hiyo yakijaribu kuwaondoa waasi wa Kiislamu wanaosaidiana na wanamgambo wa kiukoo.

Watu walioshuhudia wanasema kuwa marengo ya maduka pamoja na nyumba nyingine katika kitongoji cha Tawfiq kaskazini ya mji huo yameungua moto na raia wachache waliokuwa wamebaki katika eneo hilo wanakimbia.

Watu kadha wameuwawa ama kujeruhiwa.

Jana Jumatano raia wengine wanane waliuwawa, na kufikisha idadi ya vifo katika muda wa wiki moja iliyopita kufikia 329.

Umoja wa mataifa umeishutumu serikali ya Somalia kwa kutoyapa nafasi makundi ya kutoa misaada kuwafikia mamia kwa maelfu ya watu wanaokimbia mapigano ambao wameweka makaazi ya muda nje ya mji wa Mogadishu.

Mratibu wa umoja wa mataifa wa misaada ya kiutu John Holmes amesema maafisa wa serikali ya mpito ya Somalia hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa makundi hayo kuweza kutoa misaada.

Kundi la ushauri la Uingereza la Chatham limeishutumu Ethiopia na Marekani kwa kuteka nyara juhudi za kimataifa za kuleta amani na kupuuzia hali tete ya jamii ya Kisomali.