1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Mapigano makali yaendelea kwa siku ya pili

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEC

Mapigano makali yanaendelea leo kwa siku ya pili mjini Mogadishu Somalia. Makombora yamevumishwa mjini humo huku milio ya risasi ikisika siku moja tu baada ya wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia kuwasaka wanamgambo mjini Mogadishu kutumia helikopta na vifaru.

Watu takriban 30 waliuwawa jana katika mapigano yaliyoelezwa kuwa makali zaidi kuwahi kutokea mjini Mogadishu tangu serikali ya mpito ilipouteka mji mkuu huo mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana.

Machafuko hayo yanafanyika wiki moja baada ya serikali ya mpito ya Somalia na viongozi wa kabila la Hawiye mjini Mogadishu kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.