MOGADISHU : Maelfu wakimbia kufuatia mapigano | Habari za Ulimwengu | DW | 25.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU : Maelfu wakimbia kufuatia mapigano

Maelfu ya raia wenye hofu wameukimbia mji mkuu wa Mogadishu hapo jana baada ya mapigano makali kati ya wanajeshi wa Ethiopia na wapiganaji wakati wa usiku kulikopelekea kuuwawa kwa watu 10.

Baadhi ya wakaazi walikuwa wakigombania kupanda mabasi madogo ya abiria wakati wengine wengi wakiwa na vifaa vya matumizi ya nyumbani wameondoka katika mji huo kwa miguu kuelekea kwenye viunga vya mji huo vyenye utulivu fulani ambako kuna uhaba wa chakula.

Watoto watanno ni miongoni mwa watu waliouwawa hapo jana kutokana na kwenda kombo kwa mashambulizi ya mizinga na risasi kati ya wanajeshi wa Ethiopia na wapiganaji.

Serikali ya Somalia na Waethiopia wanalaumu masalio ya mahkama za muungano wa Kislam kwa kuchochea umwagaji damu huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com