1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Maandamano nchini Somalia yapinga mswada wa azimio

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmd

Maelfu ya Wasomali hii leo wameandamana katika mji mkuu Mogadishu,kupinga mswada wa azimio la Umoja wa Mataifa uliopendekezwa na Marekani.Azma ya mswada huo ni kuregeza vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya Somalia mwaka 1992 na vile vile kuidhinisha kupeleka vikosi vya Kiafrika kulinda amani nchini humo.Kama wafuasi 4,000 wa Muungano wa Mahakama za Kiislamu ulio na nguvu nchini Somalia,walikusanyika kusini mwa Mogadishu,kuupinga mswada huo.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,limepanga kuujadili mswada wa azimio baadae leo hii.Mswada huo unapendekeza kutuma Somalia ujumbe wa wanajeshi 8,000 kutoka nchi za Kiafrika.Naibu kiongozi wa Baraza Kuu la Kiislamu nchini Somalia,Sheikh Abdurahman Janaqow amesema,litakuwa kosa kubwa kuidhinisha mapendekezo yaliotolewa na Marekani.