1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Kombora limeripuka karibu na kasri la rais

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJG

Kasri la rais katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu limeshambuliwa kwa makombora saa chache tu baada ya rais Abdullahi Yusuf kuhamia jengo hilo.Rais Yusuf,aliwasili Mogadishu siku moja baada ya bunge kukubali kuhamia tena mji mkuu kutoka ngome ya serikali mjini Baidoa.Maafisa wa serikali wamesema,watu 2 waliuawa katika shambulio hilo,lakini kwa mujibu wa mashahidi, idadi ni kubwa zaidi.Mapigano yameripotiwa pia katika maeneo mengine ya makazi mjini Mogadishu.