1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU: Hofu ya vita kuzuka nchini Somalia

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCl4

Ripoti kutoka Somalia zinasema mapigano makali yamezuka kati ya wapiganaji wa Muungano wa Kiislamu na wanajeshi wa Kisomali na wa Kiethiopia wanaolinda mji wa Baidoa ambako serikali ya mpito ina makao yake.Mapigano hayo mapya ni mfululizo wa mapambano madogo yaliyozuka kati ya pande hizo mbili katika majuma ya hivi karibuni na kuzusha hofu ya uwezekano wa vita kuripuka na kuzitumbukiza nchi za jirani katika mgogoro huo.Mapigano hayo yametokea siku mbili baada ya Umoja wa Mataifa kuidhinisha mipango ya kutuma Somalia vikosi vya amani,hatua ambayo inapingwa na Muungano wa Kiislamu.