1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOGADISHU : Bomu lauwa wanane Baidoa

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnu

Hali ya mvutano nchini Somalia yazidi kuongezeka baada ya bomu kuripuka kwenye gari huko Baidoa na kuuwa watu wanane katika kituo cha ukaguzi karibu na makao makuu ya serikali ya mpito dhaifu inayotambuliwa kimataifa.

Serikali hiyo inaulaumu Muungano wa Mahkama za Kiislam wenye makao yake makuu mjini Mogadishu unaoungwa mkono na kundi la Al Qaeda kwa kuhusika na mripuko huo.

Msemaji wa Muungano wa Mahkama hizo za Kiislam amekanusha kuhusika na mripuko huo.

Shambulio hilo limekuja masaa machache baada ya bunge katika nchi jirani ya Ethiopia kuidhinisha serikali yake kuchukuwa hatua zote zinazohitajika kuzima uvamizi dhidi ya nchi hiyo.

Uongozi wa Kiislam katika miezi ya hivi karibuni umeishutumu Ethiopia kwa kutuma vikosi nchini Somalia. Ethiopia imekanusha jambo hilo lakini imekiri kutuma washauri wa kijeshi.