1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mmoja wa washukiwa wa utekaji nyara wa watotowa kiafrika atolewa mahakamani Chad akiwa hoi

24 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfrt

N’DJAMENA:

Muuguzi mmoja wa kifaransa,na wenzake watano wanaokabiliwa na kesi ya kuwateka nyara watoto 103 wa Kiafrika,ameondolewa mahakamni leo akiwa hoi baada ya kugomea chakula kwa mda mrefu.

Nadia Merimi pamoja na wenzake wengine watano wa shirika la misaada la Zoes Ark,mapema mwezi huu ,walianza mgomo wa kutokula kutokana na hali waliomo kwa sasa.

Watu sita wanadai kuwa walitaka kuwaokoa watoto maskini kutoka Sudan na kuwapeleka Ulaya.

Wendesha mashtaka wanasema watoto wote ni raia wa Chad waishio na familia zao.

Raia wengi wa Chad nao wanakabiliwa na kesi hiyo.Ikiwa watapatikana na hatia ,wafanya kazi hao wa kifaransa hawatatekeleza adhabu yao nchini Chad bali Ufaransa.