1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mmoja wa walioshikiliwa katika gereza la Guantamo Bay kuachiliwa huru

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChRS

CANBERA:

Baada ya kushikiliwa kwa kipindi cha miaka saba katika jela la Guantanamo Bay na nchini Australia, David Hicks alieunga mkono magaidi, ataachiliwa huru jumamosi.Serikali ya Australia imemuwekea masharti magumu ya kutembea.Hicks ndie mshukiwa wa kwanza wa ugaidi kuhukumiwa na mahakama ya kijeshi ya Marekani katika gereza la Guantanamo Bay Cuba, wakati alipokiri kosa lake mwezi Machi la kusaidia Al-Qaida. Aidha alikiri kuhudhuria kambi za mafunzo ya kigaidi nchini Pakistan.