1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mmea wa Jatrofa wanyauka kabla hata ya kuzaa matunda ya kiuchumi

Abdu Said Mtullya28 Februari 2011

Mradi wa Jetrofa wanyauka kabla hata ya kuanza kuchipua nchini Msumbiji.

https://p.dw.com/p/10Qti
Mmea wa Jatrofa unaotumika kwa ajili ya kuzalishia nishati.Picha: DW/ Martin Vogl

Maratajio makubwa yaliambatanishwa na uzalishaji wa nishati kwa kutumia mmea unaoitwa Jatrofa.Pamoja na manufaa mengine mradi huo ungelichangia katika kulinda tabia nchi na kupunguza matumizi ya nishati za jadi kama vile mafuta.Lakini mradi huo ulianza kunyauka badala ya kumea nchini Msumbiji.

Matumaini yalikuwa makubwa juu ya mmea huo wa Jatrofa hasa kwa kuzingatia kwamba ungelitumiwa katika kuzalisha nishati wakati ambapo nishati za jadi kama mafuta zinaanza kupungua.Mmea huo pia ulijenga matumaini juu ya kuwapa wakulima mustakabal mzuri.

Duniani kote,serikali, mashirika ya kimataifa na taasisi za utafiti ziliuambatanisha mmea wa Jatrofa na mustakabal wa uhakika.Nchini Msumbiji Rais wa nchi hiyo Armando Guebuza alijihusisha na mradi huo, kwa kuanza kilimo cha Jatrofa kwa ajili ya kutoa malighali ya kuzalishia diseli.

Mtu alitarajia kuiona miti ya Jatrofa nchini Msumbiji kote, kuanzia Maputo, kaskazini mwa Msumbiji hadi katika jimbo la Nyasa kaskazini mwa nchi hiyo. Lakini mradi huo ulinyauka kabla hata ya kuanza kuota.

Hata kampuni ya Ujerumani Elaion haikuvuna ilichotarajia kutoka kwenye mradi huo wa Jatrofa- mmea ulioingizwa barani Afrika kutoka Amerika ya Kusini.Kampuni hiyo ya Ujerumani ilianza kuutekeleza mradi huo kwa kilimo cha hekta 1000 katika mji wa Beira.

Meneja wa mradi Alexander von Gablenz ameeleza kuwa Mradi wa Jatrofa haukuleta manufaa kiuchumi kwa kampuni yake.Kwa mfano mwaka jana, katika shamba lao ,hekta 50 hazikumea jani hata moja.

Baada ya kutokea hali hiyo, meneja huyo bwana Alexander von Gablenz ameeleza kuwa mradi wao haukuwa na manufaa yoyote.Amesema , tatizo la Jatrofa ni ule muda wa kusubiri. Zao hilo siyo sawa na minazi ambapo mtu anasubiri kuona matunda baada ya muda fulani. Mmea wa Jatrofa hauleti mavuno makubwa. Meneja von Gablenz amesema mtu anaekeza vitega uchumi kwa kiwango kikubwa lakini anavuna matunda kidogo sana : Mara nyingine mtu hapati hata nusu au robo ya alichoekeza.

Hapo awali mmea wa Jatrofa ulistaajabiwa sana. Ulistawi pia katika sehemu ambazo hazikuwa na rutuba nyingi.Mti huo ulisifiwa kuwa sugu dhidi ya vijidudu na magonjwa na kwamba hauhitaji kumwagiliwa maji. Kwa hiyo palikuwa na imani kwamba mti huo ulikuwa nyumbani katika mazingira ya Afrika.

Lakini Thomas Selemane wa shirika la ulinzi wa mazingira nchini Msumbiji amesema hizo zote zinazotolewa juu ya Jatrofa ni hadithi.Mnamo mwaka wa 2009 bwana Selemane alifanya uchunguzi wa miti ya Jatrofa katika mashamba mbalimbali.Amesema Jatrofa sawa na migomba au pamba lazima iangaliwe. Lazima imwagiliwe maji na kwa sababu miti hiyo pia inashambuliwa na vijidudu inapaswa kutiwa dawa.

Mwandishi/ Johannes Beck, /DW-intern/

Tafsiri/Mtullya Abdu/

Mhariri/ Abdul-Rahman