1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlima mmoja walipuka Chile

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjIj

SANTIAGO:

Nchini Chile watu kadhaa wakiwemo watalii wamehamishwa kutoka eneo la karibu na mlima wa Llaima ambao umeanza kutoa volkeno.

Mlima huo ulianza kutoa moto jumanne.Mawe ya moto pamoja na moto vilevile vimekuwa vikipaa zaidi ya mita 1,000 juu ya Volkeno hiyo.Watafiti wanahofu kuwa milipuko mingine ya hapo baadae inaweza kuwa ya nguvu zaidi.Llaima unapatikana umbali wa kilomita 700 kusini mwa mji mkuu wa Santiago de Chile na unachukuliwa kama mlima wa volkano ulio hai zaidi katika kanda ya Amerika ya Kusini. Mlima huo umelipuka mara 60 na mlipuko wa mwisho mkali ulitokea mwaka wa 1994 na ulidumu siku nne.