1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa pili kati ya India na Afrika wafanyika leo Addis Ababa

24 Mei 2011

India inajaribu kuongeza ushawishi wake kiuchumi barani Afrika na pia kutafuta kuungwa mkono azma yake ya kuwa na kiti cha kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/11MVQ
Waziri mkuu wa India, Manmohan SinghPicha: picture-alliance/Bildfunk

Mkutano wa pili wa pamoja kati ya India na Afrika unafanyika leo mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo unalenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi kati ya India na bara la Afrika. Hapo jana Jumatatu India ilisaini makubaliano na Umoja wa Afrika wa kujenga vituo 14 vya mafunzo katika nchi mbalimbali wanachama wa Umoja wa Afrika. Hayo yanafanyikia wakati wa ziara ya siku sita ya Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh barani Afrika, ambapo hii leo yuko mjini Addis Ababa, akiahidi msaada wa maendeleo kwa mabadilishano na mikataba ya kibiashara ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi wa nchi yake. Waziri mkuu Manmohan Singh anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam nchini nchini Tanzania keshokutwa Alhamisi.