1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa pande 4 juu ya Mashariki ya Kati Berlin

Mkutano wa amani juu ya mashariki ya kati wafanyika leo Berlin chini ya mwenyekiti wa UU Bibi Angela Merkel.

Leo jumatano zinakutana mjini Berlin,Ujerumani, zile pande 4 zinazohusika na mzozo wa Mashariki ya kati-Marekani,Russia,Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.Kikao hiki cha leo kinatathmini matokeo ya mkutano wa hivi majuzi wa pande 3 mjini Jeruselem kati ya waziri wa nje wa Marekani Dr.C.Rice,waziri-mkuu wa Israel, Ehud Olmert na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas.

Ramadhan Ali na ripoti zaidi:

Kuwa kundi la pande 4 juu ya mzozo wa Mashariki ya Kati linakutana kwa mara ya pili mnamo muda wa wiki chache tu anasema Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani hiyo ni mafanikio.Kimsingi lakini, upatanishi wa kundi hilo haujafika mbali kwa vile Wapalestina wameshindwa hadi sasa kutimiza sharti la mazungumzo na Israel: nalo ni:

1-O-Ton, Merkel (dt.)

“waachana na matumizi ya nguvu,walitambue dola la Israel na waheshimu mapatano yaliofikiwa hadi sasa.”

Ingawa chama cha HAMAS chini ya waziri mkuu Ismail Haniya na FATAH chini ya rais Mahmoud Abbas vilifikia suluhu wiki 2 zilizopita huko Mecca kuunda seriali ya umoja wa Taifa,waliweza tu hapo kuzima machafuko yao ya umwagaji damu ,lakini hawakutimiza sharti la mazungumzo na Israel.Kwani, chama cha HAMAS klinaendelea kutoitambua dola ya Israel na kitabakia kushika wadhifa wa waziri mkuu na wizara nyingi zitabakia mikononi mwao.

Hatahivyo, Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani hakuacha kutoa pongezi kuwa maafikiano hayo kati ya Hamas na Fatah yanatia moyo:

2-O-Ton, Merkel (dt)

“kuna matokeo ya Mecca na tuyaangalie kama hatua ya kwanza kuelekea njia barabara.”

Marekani imetathmini mafikiano ya Mecca kwa shaka shaka:

Waziri wa nje wa Marekani dr.C.Rice anadai maafikiano baina ya Hamas na FATAH yameweka zaidi pingamizi katika utaratibu wa amani kuliko kurahisisha .Na mazungumzo alioendesha yeye kati ya Bw.Abbas na waziri mkuu wa Israel Olmert yamethibitisha hayo.

Licha ya hivyo, Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani anatumai juhudi za pande 4 juu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati ,hazitaKUWA ZA BURE:

Anasema kuwa, umbo la pande hizo 4-Marekani,Russia,UM na UU linaonesha tena kile anachokiona ni muhimu sana –nacho ni kuwa wanajongeleana ,wanayashughulukia mambo kwa pamoja na wanatoa ishara ya pamoja te na huko huko Mashariki ya kati.

Kundi hili la pande 4 juu ya Masharikiya kati linapokutana leo mjini Berlin akihudhuria miongoni mwa wengine Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na waziri wa nje wa Marekani Dr.Rice,haliwezi kuleta au kulazimisha maafikiano kati ya wanaohusika-alibainisha Kanzela Merkel wa Ujerumani.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com