1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Opec

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIly

RIYADH:

Viongozi wenye siasa kali na wale wastani ndani ya Jumuiya ya nchi zinazosafirisha mafuta ulimwenguni (OPEC) wamegawika mno iwapo watumie mafuta yao kama silaha ya kisiasa kama alivyopendekeza rais Hugo Chavez wa Venezuela.

Mfalme Abdullah wa saudi Arabia ameukaripia mwito huo wa Chavez.

Viongozi hao wabainika wameungana katika kutetea bei ya juu ya mafuta ya poetroli iliopo wakati huu na kufikia rekodi ya hadi dala 100 kwa pipa.

Rais Chavez alitoa pia onyo kwamba bei ya mafuta yaweza hata kupanda na kufikia dala 200 kwa pipa endapo Marekani ikiihujumu Iran,nchi ya pili itoayo mafuta kwa wingi katika jumuiya ya OPEC.

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ambae nchi yake ni muuzaji mkubwa kabisa wa mafuta duniani, na mshirika wa chanda na pete wa Marekani, amesisitiza kuwa „mafuta yasitumike kama chjombo cha migogoro.“