1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa nchi zisizofungamana na upande wowote kumalizika leo

16 Julai 2009

Mkutano wa kilele wa 15 wa nchi zisizofungamana na upande wowote unatarajiwa kumalizika leo huko Sharm el-Sheikh Misri.Umoja huo ulianzishwa wakati wa enzi za vita baridi.

https://p.dw.com/p/Iqgj
NAM Gipfel in Ägypten 2009
Nembo ya Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande wowote(NAM)

Viongozi waliyokuwa waasisi wa kuanzishwa kwa umoja huo ni pamoja na aliyekuwa Rais wa Gamal Abdul Nasser wa Misri, Waziri Mkuu wa India, Jawaharlal Nehru wa India, Ahmed Sukarno wa Indonesia, Joseph Tito wa iliyokuwa Yugoslavia pamoja na Kwame Nkrumah wa Ghana

Malengo ya kuanzishwa kwa umoja huo ambao ni wa tatu kati ya mashariki na magharibi yalikuwa ni kuwasaidia wanachama wake kujitawala kiuchumi na kijamii.Kwa sasa umoja huo una wanachama 118.

Ilikuwa katika mkutano uliyofanyika Bandung Indonesia mwezi April mwaka 1955 ambapo viongozi 25 wa nchi na serikali za mwanzo baada ya ukoloni, walipoanzisha harakati za kuundwa kwa umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote.

Kile kinachoonekana katika dunia ya siasa za sasa, ni chanzo cha kuanzishwa kwa kundi la umoja huo.

Hata hivyo vita baridi kati ya NATO na kundi la mkataba wa Warsaw yaani Urusi na washirika wake, mara zote limekuwa ni suala likiubadili mwelekeo wa umoja huo.

Pande zote mbili zimekuwa zikipingana.Mataifa ya Afrika yaliyokuwa yakitawaliwa na yale ya Asia yaliyoanzishwa katika miaka ya 50 baada ya kujipatia uhuru wao, na mfumo wake wa siasa yamepata mafanikio makubwa na mengine kidogo.

Katika mkutano huo wa Bandung vifungu kumi vya sheria viliwasilishwa ambavyo vililazimika kuendelea kuwepo hadi katika miaka 1990.

Sheria hizo ni pamoja na kuheshimu utaifa na mifumo ya kisiasa ya mataifa yote, usawa watu wa rangi zote na utaifa, haki za binaadamu kwa kufuata makubaliano ya kimataifa pamoja na kutafuta suluhisho la mizozo yote kiurafiki kwa idhini ya Umoja wa Mataifa, bila kuchagiza au kuunda ushirika.

Katika mkutano wa kuanzishwa rasmi kwa umoja huo mwaka 1961 mjini Belgrade Yugoslavia, nchi 25 ziliudhuria.Lakini katika miongo kadhaa iliyofuatia mataifa zaidi na zaidi takriban yote ya Afrika na Asia yalijiunga na umoja huo wa nchi zisizofungamana na upande wowote.

Ilikubaliwa kutambua wazi kuwa ni kuanzishwa kwa ushirikiano na siyo shirikisho, kuweka wazi kuwa ugumu, na urasimu katika utendaji ni lazima vizuiwe.

Hata hivyo ushirika huo wa nchi zisizofungamana na upande wowote umeonekana kutoa mchango katika siasa za sasa za kimataifa.

Katika ushiriki wake huo miongoni mwao ni tukio la kusikitisha la wakati wa vita baridi ambapo August mwaka 1961 Ujerumani iligawanya na kuundwa kwa iliyokuwa Ujerumani Mashariki, kujengwa ukuta mkubwa wa Berlin uliyoitenganisha na Ulaya.

Christian Wagner kutoka taasisi ya sayansi na siasa mjini Berlin anasema kuwa katika hali ya siasa za sasa ushirikiano huo ulikuwa ni kundi la tatu,kutoka lile la mrengo wa mashariki na la mrengo wa magharibi.

"Hii hata hivyo kwa mtizamo wa mchanganyiko wa mataifa tofauti tofauti wanachama ni mkakati ambao haujaonesha kufanikiwa. Na ndiyo maana vile vile mpaka sasa mafaniko kidogo ndiyo yanaonekana.mara zote katika muundo wa mashirika ya kimataifa wamekuwa wakitafuta kuwa na malengo ya pamoja, kwa mfano kuleta maendeleo ya kudumu au kuleta mageuzi katika Umoja wa Mataifa, lakini malengo hayo yaliishia katika kauli tupu Jumuiya hiyo haina malengo thabiti ya kuonesha´´.

Katika mkutano wa kilele wa 15 wa umoja huo,unaomalizika leo huko Misri wakuu wa nchi zaidi ya 50 waliangazia zaidi masuala ya uchumi hususani mparaganyiko wa uchumi uliyoikumba dunia.

Mwandishi:Daphne Grathwohl/Aboubakary Liongo

Mhariri:Abdul Mtullya