1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na India

Mohammed Abdul-Rahman30 Novemba 2007

Pande hizo mbili zasaini mikataba katika sekta ya sayansi, ufundi na ushirikiano wa maendeleo na zina azma ya kufikia makubaliano ya biashara huria ifikapo 2008.

https://p.dw.com/p/CVBj
Waziri mkuu wa India Manmohan Singh.Picha: AP

Akizungumza na waandishi habari mjini New Delhi, Waziri mkuu wa India Manmohan Singh alisema kwamba wanatarajia kwamba hadi utakapofanyika mkutano ujao wa kilele, watakua tayari katika njia ya kukamilisha makubaliano hayo ya biashara huria .

Kwa upande wake wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya Jose Manuel Barosso, akasema wanaamini kwamba mkataba wa biashara huria utakua mkubwa na kwa hakika sehemu kubwa ya mazungumzo ya leo ilikua ni juu ya biashara.

Taarifa ya ujumbe wa umoja wa ulaya wenye wanacahama 27,ilisema mkutano huo wa nane wa kilele kati ya Umoja wa ulaya na India unakusudiwa kufikia mkakati wa ushirikiano wa karibu zaidi na kuimairisha ushirikiano katika sekta ya nishati, mabadiliko ya hali ya hewa, na mazungungumzo ya shirika la biashara duniani –WTO.

Awali mkuu wa ujumbe wa halmashauri kuu ya ulaya nchini India Bibi Daniele Smadja alisema,Biashara kati ya umoja wa ulaya na Indian ,zaidi ya euro bilioni moja kwa wiki, lakini bado haijafikia kiwango chake kinachotarajiwa.

Maafisa kutoka pande zote mbili wamesisitiza leo juu ya haja ya kukamilishwa mkataba huo ifikapo mwaka ujao. Matumaini yakitajwa pia na kamishna wa Umoja wa ulaya anayehusika na biashara Peter Mandelson.

Waziri mkuu Singh na Bw Barosso walikua na mazungumzo asubuhi pamoja na wajumbe wao wakiwemo Waziri wa mambo ya nchi za nje wa India Pranab Mukherjee. Waziri mkuu wa Ureno Jose Socrates ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa sasa wa umoja wa ulaya, wadhifa unaozunguka kila baada ya miezi sita miongoni mwa nchi wanachama , pia alihudhuria mazungumzo hayo.

Bw Barosso aligusia katika taarifa yake katika mkesha wa mkutano huo kwamba India na Umoja wa ulaya- demokrasia mbili kuu duniani- zinaweza kutoa mchango wa manufaa katika kutatua changamoto zinazoukabili ulimwengu kama vile amani na usalama, utawala bora na mabadiliko ya hali ya hewa. Mikataba ilisainiwa leo katika nyanja

Katika uwanja wa kisiasa kikao hicho kilizingatia juu ya hali nchini Nepal ambapo pande zote mbili zimesikitishwa na hatua ya kuchelewesha uchaguzi mkuu, hali nchini Sri Lanka na Pakistan, mbali na masuala ya Afrika na Mashariki ya kati.