1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa nchi nane tajiri duniani-Mahojiano

Othman, Miraji/Ali Attas7 Julai 2008

Mahojiano juu ya mkutano wa kilele wa nchi 8 tajiri duniani.

https://p.dw.com/p/EXqL
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akipokewa na waziri mkuu wa Japan, Yasuo Fukuda, katika mkutano wa kilele wa nchi nane tajiri duniani huko Toyako, Japan.Picha: AP

Viongozi wa nchi nane zilizo tajiri duniani jana walihimizwa watende zaidi kwa ajili ya Afrika. Majanga yanayowakumba mamilioni ya Waafrika walio katika hali ngumu ndio suala lililozagaa katika jenda ya mkutano huo huko Toyako, Japan, pale wakuu hao walipokutana uso kwa uso na wenziwao wa kutokea Algeria,Ethiopia, Ghana, Nigeria, Senegal, Tanzania na Afrika Kusini. Wakuu wa nchi za Kiafrika kwa pamoja waliwahimiza viongozi wa kikundi cha nchi nane zinazoongoza kiviwanda duniani wasirejee nyuma katika hadi zao walizotoa hapo kabla kungeza misaada kwa ajili ya Bara la Afrika.

Othman Miraji amezungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Ali Attas, anayefuatiliza mkutano huo huko Japan, na alitaka kujuwa kama kuna ishara zozote hadi sasa zinazoashiria kwamba Afrika itanufaika na mkusanyiko huo: