1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani

1 Mei 2007

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani akiwa mwenyekiti wa UU,yupo Washington kwa mazungumzo ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya Marekani na UU.

https://p.dw.com/p/CHF6
Merkel na Bush
Merkel na BushPicha: AP

Katika mkutano wa kilele baina ya Umoja wa Ulaya na Marekani mjini Washington,Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, akiwa Rais wa sasa wa UU , Jose Barroso, rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya kwa upande mmoja na rais George Bush wa Marekani kwa upande wapili, wamesisitiza umuhimu wa usuhuba mwema wa kiuchumi kati ya pande zao mbili.

Endapo vipimo na daraja za UU na Marekani zikikubalika na kila upande- mfano katika viwanda vya magari na madawa,basi viwanda hivyo na wanunuzi itanufaika.Hii ni kwa kuwa bidhaa hizo bei zake zitakuwa nafuu zaidi kwa wateja.

Ni fikra hii ilio nyuma ya ya mapatano ya biashara yaliofikiwa kati ya pande hizo mbili za bahari ya Atlantik .Mapatano hayo yanagusia sekta nyingi,mfano masoko ya fedha,sekta ya nishati na huduma.Mapatano hayo lakini, hayaegemi kuheshimika kisheria.

Kanzela Angela Merkel ,mwenyekiti wa sasa wa UU anasema:

“Ninaungamkono na nafurahia kuona pambezoni mwa mkutano huu,mazungumzo ya kibiashara yamefanyika-mazungumzo ambayo yanapaswa bila shaka, kufanywa na pande mbali mbali.

Nadhani, ni muhimu sana kutambua ushirikiano kati ya pande mbili za bahari ya Atlantik, hayalengwi dhidi ya biashara kati ya pande mbali mbali,bali kinyume chake.”

Katika mkutano huu huko Washington, pande zote mbili zimesisitiza hapa kuwa kama hapo kabla ipo bado hamu kuona duru ya Doha ya mazungumzo juu ya biashara ulimwenguni inafanikiwa.

Mapatano ya misafara ya ndege yaliotiwa saini kati ya UU na Marekani yanalazimisha kuheshimiwa na kila upande.

Mapatano hayo miongoni mwa mambo mengine yanaingiza kuanzia Machi 30,mwakani,mashirika ya ndege ya Marekani nay a Ulaya yanaruhusa ya kusafiri katika viwanja vyote vya ndege vya mwenzake.

Kuhusu maafikiano juu ya kupiga vita uchafuzi wa hali ya hewa,pande zote mbili zabainika kuridhika.

Hatahivyo, mapüatano hayo hayakuweka kipimo maallumu cha juu kabisa kukiukwa kuzuwia moshi unaochafua hewa kinyume na vile nchi za UU zingependelea.Tangu kanzela Angela Merkel hata rais wa Tume ya Ulaya Barroso,wanayaangalia ni hatua moja mbele.

Bi Angela Merkel:

2.”Tumegundua mengi ya kushirikiana; na msingi mmojawapo ulikuwa kuchukua dhamana Marekani ,kuunda vinu vya nishati ya bio hadi ifikapo mwaka 2020.Kwa lengo hilo, tutakuwa na vipimo na soko la pamoja ambalo kwa maoni yangu taftishi zitasukuma mbele mradi huo.”

Mada nyengine nyingi zilizungumzwa katika mkutano huu wa kilele baina ya UU na Marekani.

Kwa mfano jibu kali la rais wa Russia,Wladmir Putin juu ya mpango wa Marekani wa kujenga kinga ya makombora Ulaya ya kati.Rais Bush alitaja kuwa, Kanzela Merkel alimshauri bora kuzungumza binafsi na rais Putin.Bush akasema atalifuata pendeklezo hilo na ndio maana amemtuma waziri wake wa ulinzi mjini Moscow.

“Lengo letu ni kuwaambia warusi, wafikirie nao kushiriki katika mradi huu wa ulinzi.Kwani, pia ni kwa manufaa yao kuwa kinga hiyo, itaizuwia Iran kushambulia kwa kutumia makombora yake.”

Mbali na hayo, wanasiasa wa pande hizo mbili waliafikiana kusaka ufumbuzi wa mizozo kama Afghanistan,Kosovo,Irak na Mashariki ya kati bila kusahau mzozo wa Dafur.