1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa IAEA waanza leo

7 Septemba 2009

Shirika la Nguvu za Atomiki la Kimataifa IAEA limeanza mkutano wake hii leo mjini Vienna Austria.

https://p.dw.com/p/JTx7
Mkurugenzi mpya wa IAEA, Yukiya AmanoPicha: AP

Mkutano huo utajadili madai kwamba Iran ilifanya utafiti ulio na azma ya kutengeza mabomu ya nuklia vilevile madai kwamba Syria ilikuwa na harakati za kutengeza kinu cha nuklia kabla ya kuvamiwa na Israel mwaka 2007.

Shirika hilo lililo na nchi 35 wanachama linahusika na usimamizi wa kusambaa kwa silaha na teknolojia ya nuklia.

Kile  kilicho  muhimu  kinalindwa  sana. Kwa  idara   hii  ya uchunguzi, wafanyakazi  wanachunguza   maeneo  ya kinuklia  kutoka  duniani  kote  ili  kuweza  kuweka  pamoja uchunguzi  wao. Iwapo  mtu  anataka  kuingia  katika ukumbi  huo  kwanza  lazima  atoe  taarifa   na  kisha atafunguliwa  milango  maalum  ya  ukumbi  huo. Wachunguzi  hapa  wanawajibika  tu  kufanyakazi  zao ngumu  za  siri  na  sio  kuzungumza. Mwalimu  wao  Jean-Maurice  Crete  amekuwa  kwa  miaka  kadha  akifanyakazi kama  mtaalamu  wa  fizikia  ya   kinuklia  katika   nyambizi iliyo  na  silaha  za  kinuklia  ya  jeshi  la Ufaransa. Anafahamu  mengi  kuhusu  vinu  vya  kinuklia,  lakini  hata silaha  za  kinuklia. Na  anafahamu  kile  ambacho wachunguzi  wanatarajia, wakati  akiwa  peke yake  popote pale  katika  bara  la  Asia  ama  Amerika  ya  kusini chombo  chake  kinaweza  kuleta  kutoka  katika  kituo  cha kinuklia  na  kuwaeleza  wahandisi  wadadisi    kilichomo katika  kamera zinazoangalia  vinu  hivyo.

Karibu  wachunguzi  300  wanaangalia  duniani  kote  kiasi cha  maeneo  1,100. Malalamiko  mengi  ni  kuhusu  tatizo la  wataalamu  vijana, vijana  ambao  wanautaalamu  wa fizikia  ya  kinuklia  ni  wachache, na  katika  vituo  vya kinuklia  wanapata  fedha  zaidi. Katika  shirika  la  IAEA wanakuja  tu  wale  ambao  wana  nia  halisi, anasema Jean-Maurice Crete. Katika  idara  yake  kila  mwaka anapata  fedha  nyingi,  kama   nusu  ya  gharama  ya ndege  ya  kivita. Ni  kiasi  gani  kinatumika  kwa  ajili  ya amani  ya  dunia? Ukosefu  huu  wa  fedha, haukumshitua pia  mshindi  wa  tuzo  ya  amani  ya  Nobel, ambayo aliipata  mkuu  wa  shirika  hilo  2005. Na  huo  ndio ulikuwa  ushindi  mkubwa  wa  mkurugenzi  mkuu  wa IAEA  Mohammed el Baradei, na  kusababisha  kupata zawadi, ambapo  alisaidia  kupunguza  nguvu  za  madai ya  rais  George  W. Bush     kuwa  Iraq  inamiliki   silaha za  maangamizi.

Mwanasheria  huyo  kutoka  Misr  anaondoka  katika wadhifa  wa  mkurugenzi  mkuu  wa  shirika  hilo  mwezi Novemba  mwaka  huu.

Kwa  kuaga  kwa  mara  nyingine  tena  ameonya kutolifanya  shirika  hilo dhaifu  zaidi. IAEA  inahitaji  haraka kiasi  cha  Euro  milioni  80  ili  kufanya  ukarabati  muhimu , na  pia  kuwapata  wafanyakazi  wapya  kwa  ajili  ya  kazi ngumu  ya  shirika  hilo. Baradei  ameeleza  uzoefu  wake kwa  msisitizo  mkubwa.

´´Uwezo  wetu  wa  kutekeleza  mfumo  wa  tathmini  ya kinuklia  na  kugundua uwezekano  wa  udanganyifu  wa mada  za  kinuklia  na  shughuli  za  kinuklia  ambazo hazikuwekwa  wazi, tayari  uko  mashakani. Kwa  sababu kwa  mfano  maabara  zetu  za  uchunguzi  ni  za  kizamani na  tunakosa  uwezo  wa  kupata  picha  rasmi  za satalite´´.

Bila  ya  kupata  fedha  za  nyongeza  hali  hii  itakuwa mbaya  zaidi. Nafasi  ya  kurejewa  kwa  maafa  kama  ya Chernoble itakuwa  kubwa  zaidi, iwapo  upungufu mkubwa  wa  wafanyakazi  katika  mpango  wa  usalama wa  kinuklia  hautaangaliwa.

Mwandishi: Eberhard Nembach/ZR/ Sekione  Kitojo.

Mhariri :Aboubakary  Liongo.