1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Hamas na Fatah waendelea mjini Makkah

Josephat Charo7 Februari 2007

Viongozi wa vyama hasimu nchini Palestina wameanza mazungumzo muhimu mjini Makkah Saudi Arabia hii leo, wakiapa kufikia makubalianoya kufgawana madaraka na kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Palestina.

https://p.dw.com/p/CHKZ
Haniyah (kushoto) na Abbas mjini Makkah Saudi Arabia
Haniyah (kushoto) na Abbas mjini Makkah Saudi ArabiaPicha: AP

Mkutano wa mjini Makkah ni muhimu kwani makubaliano yatakayofikiwa yatafungua mlango wa kuanza tena mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Israel na Palestina. Wapelstina wengi wana hofu kwamba mapigano mabaya zaidi baina ya chama cha Hamas na chama cha Fatah yatazuka iwapo mazungumzo ya mjini Makkah yatafeli kufikia suluhu.

Kama ishara ya umoja, kiongozi wa chama cha Hamas, anayeishi uhamishoni, Khaled Mashaal na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kiongozi wa chama cha Fatah walisafiri kwenda Makkah kutumia motokaa moja katika siku ya kwanza ya mazungumzo ambayo maofisa wa Saudia na Palestina wanasema yatakuwa ya kina na marefu na yataendelea mpaka suluhisho lipatikane.

Mshauri wa rais Abbas anayehusika na vyombo vya habari, Nabil Amr amesema wana matumaini makubalianoy atafikiwoa hivi karibuni.

´Tuna matumaini kwamba katika kipindi kifupi kijacho makubaliano yatafikiwa kuhusu mzozo wa kisiasa wa kuunda serikali ya umoja wa taifa na baadaye kutangazwa kwa serikali hii. Katika mazungumzo yetu hapa Makka tutajaribu kulifikia lengo hilo.´

Tumekuja hapa tukubaliane na hatuna chaguo lengine bali kukubaliana, amesema Mashaal wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mazungumzo hayo kwenye ikulu ya mfalme wa Saudi Arabia mjini Makkah. Rais Abbas kwa upande wake ameapa hawataondoka mji mtakatifu wa Makkah mpaka watakapokubaliana kuhusu mambo yote mazuri pamoja na baraka za mwenyezi Mungu. Amewaambia Wapalestina watarajie habari njema kutoka mkutano huo wa mjini Makkah na kueleza matumaini yake kwamba mkutano huo hautakuwa wa maneno matupu.

Rais Abbas amesema wanataka kuunda serikali ya umoja wa taifa itakayomaliza machafuko na kuzuia umwagikaji damu. Siku zilizopita zimekuwa mbaya na Mungu aepushe mbali zisirudi tena. Limekuwa janga kubwa lisilotakiwa kurudiwa tena, amesema rais Abbas mjini Makkah.

Alipoulizwa jukumu la Saudi Arabia katika mkutnao wa Makkah, Nabil Amr amesema maofisa wa Saudia hawashiriki moja kwa moja katikama zungumzo hayo.

´Wametuachia uhuru wa kujadili. Tukihitaji msaada wao tutawomba watusaidie. Na hapo wataangalia makubaliano tuliyofikia na kuzihimiza pande zoze zifikie muafaka. Wako tayari kusaidia wakitakiwa kufanya hivyo. Tunaweza kusema Wasaudi wana jukumu muhimu katika mkutano huu na kwa kutualika na kuwa tayari kutupa msaada ambao bila shaka tunauhitaji.´

Wakati haya yakiarifiwa, wapiganaji wametishia kufanya mashambulio ya kulipiza kisasi hii leo mjini Gaza, licha ya amri ya kusitisha mapigano na mkutano wa kumaliza uhasama kati ya Hamas na Fatah unaoendelea nchini Saudia Arabia. Wanamgambo wa chama cha Hamas wameonya watafanya mashambulio mapya ikiwa maofisa wa Fatah wanaowatuhumu kuhusika katika shambulio la wiki iliyopita dhidi ya chuo kikuu cha kiislamu wawasilishwe kwao kablaleo kumalizika.