1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa EU wakamilika bila muafaka wa hati za dhamana

24 Mei 2012

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walimaliza mkutano wao wa kilele mjini Brussels kwa kuchukua hatua muhimu za kutatua mgogoro wa kiuchumi barani humo, huku hofu ya Ugiriki kujiondoa katika kanda ya euro ikiongezeka

https://p.dw.com/p/151Ne
(L-R) Italy's Prime Minister Mario Monti, Germany's Chancellor Angela Merkel and France's President Francois Hollande attend an informal EU leaders summit in Brussels May 23, 2012. European leaders will try to breathe life into their stricken economies at a summit over dinner on Wednesday, but disagreement over the issue of mutual euro-zone bonds and whether they can alleviate two years of debt turmoil will dominate the gathering. REUTERS/Francois Lenoir (BELGIUM - Tags: POLITICS BUSINESS)
Brüssel Krisentreffen EU-Sondergipfel GriechenlandPicha: Reuters

Viongozi wengine walisisitiza umuhimu wa kupanga hafla hiyo lakini hawakutoa hatua ambazo zinaweza kuisaidia Ugiriki kusalia katika kanda hiyo. Pia suala ambalo halikushughulikiwa lilikuwa kile bara Ulaya linapaswa kufanya ili kuimarisha ukuaji wa uchumi na kurejesha imani ya wawekezaji, ambao wamesababisha gharama za ukopaji kwa nchi nyingine kufikia viwango visivyoaminika.

Mpango wa kubana matumizi ambao Ujerumani imeupigia upatu kama suluhisho kwa tatizo la Ulaya la madeni mengi ya serikali umekumbwa na ukosoaji katika nchi nyingine za sarafu ya euro.

Hati za dhamana bado suala tata
Viongozi wa nchi 27 zinazounda Umoja wa Ulaya walikubaliana kuzipa taasisi kama vile Benki ya Uwekezaji ya Ulaya jukumu la kuandaa pendekezo la ukuaji kabla ya mkutano ujao wa kilele unaopangwa mwezi Juni.

Mkutano wa EU ulijaribu kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kifedha
Mkutano wa EU ulijaribu kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kifedhaPicha: dapd

Lakini kulikuwa na ugomvi kuhusu hatua zaidi kali zinazoshinikizwa na baadhi ya viongozi wanaohudhuria kikao hicho, kama vile kutoa hati dhamana kwa pamoja kama njia moja ya kupunguza gharama za kukopa kwa mataifa yaliyo na madeni makubwa miongoni mwa nchi 17 zinazotumia sarafu ya euro.

Dhana kuwa viongozi wa Ulaya wanakosa nia ya kisiasa ya kuyakabili matatizo ya kifedha na kiuchumi barani humo imeyafanya masoko ya fedha kuyumba katika wiki kadha azilizopita. Mdororo wa kiuchumi unasambaa. Benki ziko chini ya shinikizo. Wasiwasi ni kuwa ikiwa Ugiriki haitaokolewa, mataifa mengine kama vile Ureno na Uhispania huenda yakatumbukia katika tatizo kama hilo. Waziri Mkuu wa Luxembourg Jean-Claude Juncker anasema nchi za sarafu ya euro ni sharti zizingatie aina yote ya matukio, lakini akasisitiza kuwa wazo lililopo kwa sasa ni kuwa Ugiriki itasalia katika ukanda wa sarafu ya euro. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema baada ya mkutano huo kuwa wanataka Ugiriki isalie katika kanda ya euro.

Ugiriki yapigiwa upatu
Lakini mkutano huo wa leo wa viongozi wa EU umekamilika bila makubaliano yoyote.

Ulikuwa mkutano wa kwanza kwa rais Ufaransa Francois Hollande
Ulikuwa mkutano wa kwanza kwa rais Ufaransa Francois HollandePicha: dapd

Taarifa ya mwisho ilisema Ugiriki ni sharti iheshimu ahadi zake na ikatilia mkazo fedha ambazo kanda ya euro na shirika la fedha la Kimataifa IMF yaliikopesha Ugiriki kama ishara ya wao kuonyesha mshikamano.

Ilisema kuwa fedha za maendeleo ya uchumi zitatumwa kwa Ugiriki. Rais wa Ufaransa Francois Hollande alisema hali hiyo inaweza kutuma ujumbe kwa masoko kuwa ukanda wa euro haushirikiani na Ugiriki.

Viongozi pia waliangazia suala tata la ikiwa nchi zinazotumia sarafu ya euro zinafaa kujweka hatarini na kukopa pesa kwa pamoja, kwa kutoa kile kinachojulikana kama hati dhamana za sarafu ya euro. Hii ina maana kuwa kila nchi huenda ikakopafedha kwa kiwango sawa, na kupunguza gharama za zile nchi zilizo na madeni. Hollande ameshinikiza suala hilo kama njia moja ya kuhakikisha kuwa mzozo kama huo hautokei tena, lakini Merkel amekataa, akihofia kuwa zinaweza kupunguza shinikizo dhidi ya serikali zilizo na madeni makubwa sana kuokoa fedha zao na kuilazimisha Ujerumani kukopa kwa viwango vya juu

Mwandishi: Bruce Amani/AP
Mhariri: Sekione Kitojo