1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa Durban haujafikia makubaliano

Afrika Kusini, mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya tabia nchi,mjini Durban,imepaswa kuwasilisha mswada mpya wa mkataba baada ya mapendekezo ya hapo awali kupingwa na nchi wanachama 154 kutoka jumla ya 194.

Delegates attend the High Level Segment of the COP 17 / CMP 7 United Nations (UN) Climate Change Conference 2011 in Durban, South Africa, 07 December 2011. The 17th session of the Congress of the Parties (COP) comprising 194 countries meeting to discuss the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) is in its High Level Segment serving as the meeting of the Parties to the Kyoto Protocol. EPA/NIC BOTHMA

Mapendekezo mapya yajadiliwa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Durban

Miongoni mwao ni nchi zinazoendelea ambazo pia zipo katika hatari kubwa sana ya kuathirika kutokana na ongezeko la joto duniani.Hata waziri wa mazingira wa Ujerumani Norbert Röttgen amesema, mswada uliopendekezwa na Afrika Kusini hautoshi. Mbali na kupendekeza kuirefusha Itifaki ya Kyoto, mswada huo vile vile unapendekeza kuwa na mkataba wa kimataifa ifikapo mwaka 2020. Lakini hakuna cho chote kilichotajwa juu ya kuwajibika kisheria. Waziri Röttgen na mkuu wa masuala ya mazingira wa Umoja wa Ulaya, Connie Hedegaard, wamesema, mwaka 2020 ni mbali mno. Wao wangependa kuwa na mkataba mpya ifikapo mwaka 2015. Bila ya kutarajiwa, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, ikiwemo Ujerumani pia, ziliungana na kundi la nchi masikini zinazoendelea pamoja na mataifa ya visiwani yanayokabiliwa na hatari kubwa ya kuathirika zaidi kutokana na ongezeko la joto duniani.

epa03026890 Norbert Roettgen, Minister of Environment of Germany speaks during the High Level Segment of the COP 17 / CMP 7 United Nations (UN) Climate Change Conference 2011 in Durban, South Africa 07 December 2011. The 17th session of the Congress of the Parties (COP) comprising 194 countries meeting to discuss the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) is in its High Level Segment serving as the meeting of the Parties to the Kyoto Protocol. EPA/NIC BOTHMA +++(c) dpa - Bildfunk+++

Waziri wa Mazingira wa Ujerumani Norbert Röttgen akihutubia mkutano wa Durban

Kiini cha mzozo huo ni njia ya kuziwajibisha kisheria nchi zinazotia saini mkataba huo na tarehe ya mkataba huo kuanza kufanya kazi. Mkakati wa Umoja wa Ulaya ni kuzishinikiza China, Marekani na India kutia saini makubaliano ya kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua mazingira. Mataifa hayo matatu ni wachafuzi wakubwa kabisa wa mazingira duniani na hakuna hata mmoja wao anaelazimika kupunguza viwango vya gesi hiyo kuambatana na Itifaki ya Kyoto. Marekani inasema, itaahidi kupunguza uzalishaji wa gesi inayochafua mazingira kuambatana na viwango vinavyotakiwa, ikiwa tu wachafuzi wengine wakuu pia watakubali kutoa ahadi kama hiyo. Lakini China na India zinasema, si haki kuyataka mataifa hayo kupunguza kwa viwango kama vile vya mataifa yaliyoendelea kiviwanda na ambayo kwa sehemu kubwa yamesababisha uchafuzi wa mazingira unaolaumiwa kuongeza ujoto duniani.

Wajumbe wengi katika mkutano huo wa wiki mbili mjini Durban, wanaamini, hakuna zaidi kitakachopatikana isipokuwa makubaliano dhaifu ya kisiasa, huku nchi zikiahidi kuanzisha majadiliano ya mkataba mpya kuhusu viwango vya gesi zinazochafua mazingira, utakaopaswa kuheshimiwa.
Mwandishi: Jeppesen,Helle/ZPR- Martin,Prema/RTRE/DPAE
Mhariri: Sekione, Kitojo

 • Tarehe 10.12.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13QHf
 • Tarehe 10.12.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13QHf

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com