Mkutano wa Annapolis | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mkutano wa Annapolis

Jaribio la mwisho lilifanyika kuziba mwanya kati ya waisraeli na wapalestina kabla kuanza kwa kikao

default

Maalfu ya wayahudi waomba dua juu ya annapolis

Wajumbe wa Palestina na wa Israel, walijadiliana usiku mzima hapo jana ili kupunguza tofauti zao kabla ya kuanza kikao cha leo juu ya mashariki ya kati ambacho rais George Bush wa Marekani, ameonya kitahitaji kila upande kujitolea kweli ili kumridhia mwenzake.

Kabla ya rais Bush hakuufungua rasmi mkutano wa Annapolis ,Maryland,maafisa wa Israel na wa kipalestina walifanya jaribio la dakika ya mwisho kuziba mwanya wa tofauti uliosalia ili waweze kutoa taarifa ya pamoja mwishoni mwa kikao hiki itakayojenga msingi wa majadiliano yatakayoanza mara tu mkutano huu umemalizika.

Mawaziri na maafisa wa hadhi ya juu kutoka nchi na mashirika 1hadi 50 –pamoja nao waziri wa nje wa Ujerumani Walther-steinmaier, nchi za kiarabu kama vile Saudi Arabia na hata Syria zisizoitambua Israel zinawakilishwa katika jaribio kubwa kabisa la George Bush la kuwaleta pamoja mahasimu hawa wakubwa wa mgogoro wa mashariki ya kati.

Rais Bush alikutana jana na viongozi kutoka pande zote mbili huko Ikulu (white House)mjini Washington,na baadae akazitaka pande zote kujitolea kweli kumridhia mwenziwe-hatua a mbayo alisema inahitajika ili kuunda dola la wapalestina litakaloishi bega kwa bega kwa amani na Israel.

Bush akasema ana matumaini katika kuyafufua mazungumzo haya ya amani baada ya kupita miaka 7 na akathibitisha tena kile wakoasiaji wamekiita masilahi yake binafsi juu ya hatima ya mazungumzo haya.

“Usiku huu, nakariri kule kujitolea kwangu binafsi na kwa niaba ya Marekani kwa wale wote watakao kuishi uhuru na kwa amani huko Mashariki ya kati.Tunasimama pamoja nanyi katika mkutano huu wa Annapolis na kupindukia hapa.”

Kwa upande mmoja Bush kama hapo kabla matarajio ya kikao hiki cha siku moja kutoyakuza.

Katika hotuba yake fupi kwenye wizara ya nje ya marekani Bush alitaja tena kwamba shabaha yake ni kuwa na dolasuluhisho la dola mbili na kuifikia shabaha hiyo kunahitaji kila upande kujitoa mhanga: "Kuifikia shabaha hii,panahitaji kuwapo majirani waliojitolea kuona amani inafikiwa baina ya Israel na dola jipya la wapalestina.Nimetiwa moyo na kuhudhuria kwa wingi kwa waakilishi wan chi za eneo hili.”

Hata waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya ndani ya wapalestina,Mahmud Abbas wameelezea nia yao ya kufikia mapatano juu ya utaratibu wa amani wa mashariki ya Kati kabla kipindi cha utawala wa George Bush kumalizika.

Wakati wa ziara yake huko Ikulu ya marekani (White House) kabla ya adhuhuri ya jana, waziri mkuu wa Israel alisema: “Mara hii hali ni tofauti ,kwani, tuna wajumbe wengi wanaoshiriki katika tukeo hili ambalo nataraji kutaibuka mwishoe utaratibu madhubuti wa mazungumzo kati yetu na wapalestina.”

Mbali na Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya,isipokua chama cha hamas, zashiriki pia Syria,Lebanon,Misri na saudi Arabia.Mahmud Abbas rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina nae alisema: “Tuna matumaini makubwa kuwa kutoka mkutano huu, hatima ya mwisho ya maswali mengi yanayo bishaniwa itaamuliwa.Maswali ambayo baadae, yatajumuishwa katika mkataba wa amani baina ya Israel na wapalestina.Mkataba utakaohakikisha usalama na utulivu.”

Wakati huo huo, mamia ya wafuasi wa kundi la Hamas linalodhibiti eneo la ukanda wa Gaza waliandamana huko Gaza kupinga mkutano wa Annapolis. Kundi la Hamas na makundi mengine madogo yenye msimamo mkali yalisema rais Mahmoud Abbas hana haki ya kuongoza mazungumzo kwa upande wa Wapalestina.

Katika mkutano uliofanyika mjini Gaza waandamanaji walitia saini taarifa ya pamoja na mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh alisema: “Wenye kuamua juu ya sheria ya taifa la Wapalestina leo wanatia saini hati inayosisitiza takwa la Wapalestina kupewa haki zao zote pamoja na kuukataa mkataba wowote unaokiuka haki hizo. Wakati huo huo wanaona makubaliano yanayofikiwa na Wapalestina wanaohudhuria mkutano huo wa kilele hayatakuwa na maana.”


Awali, kundi la Hamas lilipanga kufanya mkutano wake mwingine huko Damaskus, Syria, lakini kutokana na Syria kushiriki pia kwenye mkutano wa Annapolis ilibidi Hamas ifanye maandamano huko Gaza, eneo linalolidhibiti.


Wapalestina wengine waliandamana huko Lebanon na katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, “West Bank” ambapo mmoja wa waandamanaji aliuawa.

 • Tarehe 27.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali / Maja Dreyer
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CTgc
 • Tarehe 27.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali / Maja Dreyer
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CTgc

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com