1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Annapolis ni tukio la kihistoria

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUGR

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameridhika na matokeo ya mkutano wa kimataifa kuhusu Mashariki ya Kati uliofanywa Annapolis,nchini Marekani.Kabla ya kuondoka Marekani,Steinmeier alisema,matumani ya mkutano huo yametimia.Kwa upande mwingine,Umoja wa Ulaya umezungumzia matokeo ya kihistoria.Lakini waandishi wa habari wa Kiarabu walikuwa na maoni tofauti kuhusu matokeo ya mkutano huo.Wao wamesema,Rais wa Marekani George W.Bush ameshughulikia zaidi kuondosha mawazo ya Waarabu kutoka Israel na badala yake kuyaelekeza dhidi ya Iran.