1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa amani mashariki ya Jamhuri ya kidemokrtasi ya Kongo

Oummilkheir6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cl6C

Mkutano wa amani kwa majimbo ya kaskazini na kusini ya Kivu-katika eneo la mashariki la jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo unaanza hii leo mjini Goma.Habari hizo zimetangazwa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo askofu Appolinaire Malu Malu mjini Goma.Mkutano huo wa amani,usalama na maendeleo unafanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huru cha maziwa makuu mjini Goma.Mkutano huo unaitishwa kutokana na juhudi za rais Joseph Kabila,kwa lengo la kumaliza mivutano katika maeneo ya mpakani pamoja na Burundi na Rwanda.