1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa 55 wa Jumuiya ya Madola mjini Arusha,Tanzania

6 Oktoba 2009

<p> Mkutano wa 55 wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola, Commonwealth, unakutana mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania.

https://p.dw.com/p/K02n
Moja ya mada iliowagusa sana wajumbe katika mkutano huo ni kuanzishwa serikali za mseto kama suluhu ya kumaliza migogoro ya kisiasa inayotokana na kuvurugika kwa mazoezi ya uchaguzi barani Afrika. Suala  muhimu lilikuwa namna ya kupata muwafaka wa kukomesha vurugu na mabishano kabla na baada ya uchaguzi.

Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na Hamad Rashid Mohammed, mkuu wa upinzani katika bunge la Tanzania na mbunge wa Wawi, Kisiwani Pemba, kwa tiketi ya Chama cha CUF, kuhusu msimamo wa chama chake juu ya serikali za mseto baada ya  chaguzi katika nchi za Afrika...

Mtayarishi:Othman Miraji

Mpitiaji: Mohamed Abdulrahman