1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa Paris waanza kutekelezwa

4 Novemba 2016

Utekelezaji wa mkataba wa kihistoria unaolenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi uliosainiwa Jijini Paris, Ufaransa mwezi Desemba mwaka jana, umeanza kutekelezwa baada ya mkataba huo kuwa sheria.

https://p.dw.com/p/2S8mO
China Emissionen von Kohlendioxid
Picha: Getty Images/K. Frayer

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu haja ya msingi kwa sasa ya kupunguzwa kwa uzalishaji wa gesi chafu ili kufikia malengo ya kimataifa. 

Kwenye taarifa ya pamoja ilitolewa na maafisa wa Umoja wa Mataifa wa masuala yahusuyo hali ya hewa leo hii, wanasema binadamu wataiangalia siku hii ya kama siku ambayo dunia ilifunga milango ya majanga yanayoikumba dunia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuanza ukurasa mpya kwa maendeleo endelevu yajayo. 

Kufikiwa kwa mkataba huu ambao sasa ni sheria, kunaongeza msukumo wa nchi kuanza kujiwekea mikakati ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ili kukabiliana na ongezeko la halijoto duniani. Nchi 200 kwa pamoja zilikubaliana kupitisha mkataba huo wa Paris uliosainiwa mwaka 2015, mnamo mwezi Disemba mwaka jana, na unatajwa kama mkataba mgumu wa kidunia kando ya mkataba wa kibiashara wa Marrakesh, uliosainiwa mwaka 1994.

Mkataba wa Paris ulikabiliwa na kizingiti, katika kipindi cha mwezi Octoba wakati ambapo mataifa 5 kati ya 55 yaliyolaumiwa kusababisha uzalishaji wa gesi chafu kwa zaidi ya asilimia 55, walipoamua kwamba mkataba huo uanze kutekelezwa siku 30 baadae. Hata hivyo kuridhiwa kwa makataba huo hakukumbwa na ugumu ikilinganishwa na mikataba mingine ya kimataifa, hatua inayodhihirisha uungwaji mkono thabiti wa jumuiya ya kimataifa, ingawa takriban nchi 100 bado hazijaridhia.

Solomon Islands
Visiwa va Solomon na Russel vilivyoko Pacific. kwa pamoja vinatishiwa na kuongezeka kwa kina cha bahari kutokana na mabadiliko ya tabianchi.Picha: picture-alliance/robertharding/M. Runkel

Awali, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Stephane Dujarric ameelezea kuridhishwa kwake na hatua za kimakubaliano zilifikiwa huku akizitaja baadhi ya nchi ambazo zimejitokeza wiki hii kuunga mkono mkataba huo kuwa sheria, ambazo ni pamoja na Afrika Kusini, Jamhuri ya watu wa Korea, 

Afisa wa masuala ya hali ya hewa wa umoja wa mataifa, Patricia Espinosa amesema kwenye taarifa yake kwamba ndani ya takriban miaka 15, wanahitaji kuona upunguzwaji mkubwa wa uzalishaji wa gesi inayochafua hewa na hatua pamoja na hatua zinazofanana za kujenga jamii mpya itakayokabiliana na kuongezeka kwa hali ya mabadiliko ya tabianchi. 

Mkataba wa huu wa Paris unalenga kupunguza katika uchumi wa ulimwegu matumizi ya nishati ya mafuta ifikapo nusu ya pili ya karne, ili kuweka ukomo wa kupanda kwa wastani wa nyuzi joto duniani kwa angalau chini ya nyuzijoto 2.0. Makubaliano hayo yalianza kwa kuangazia ukanda wa Pacific, ambako kunakopatikana visiwa vingi ambavyo vinakabiliwa na kitisho cha ongezeko la kina cha bahari.

Mzunguko wa mwisho wa mazungumzo hayo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, utaanza Jumatatu ijayo mjini Marrakesh nchini Morocco ambako wawakilishi kutoka nchi mbalimbali watajaribu kuangazia namna ya kuutekeleza mkataba huo.

Mwandishi: Lilian Mtono / http://www.dw.com/en/paris-accord-on-climate-change-comes-into-effect/a-36255526/ rtre.
Mhariri: Saumu Yusuf