1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa amani wa Uganda walegalega

Kalyango Siraj11 Aprili 2008

Ujumbe wa serikali waondoka kutoka kituo cha mpaka

https://p.dw.com/p/Dg41
Wapiganaji wa Lord Resistance Army-LRA- wakiwa katika ulinzi wakati kiongozi wao Kony akikutana na wajumbe wa serikali mwaka mwaka 2007. Kiongozi wao amekataa kutia sahihi mkataba wa amaniPicha: AP Photo

Mkataba wa kumaliza vita vilivyodumu miongo miwili kaskazini mwa Uganda baada unalegalega kufuatia mhusika mkuu ,Joseph Kony,kiongozi wa kundi la waasi la Lord Resistance Army,LRA,kushindwa kutimiza ahadi yake ya kutia saini mkataba huo hiyo jana alhamisi.Sasa macho yote yanasubiriwa kuona ikiwa leo Ijumaa atafanya hivyo.

Kupata mkataba wa amani ya kudumu nchini Uganda ,kati ya serikali kuu na wahasimu wao wa kaskazini wa kundi la LRA, kunaonekana kama kumegeuka kuwa sarakasi.Hii ni kwa sababu ya ati ati kutoka kwa upande mmoja husika wa waasi wa LRA.

Kiongozi wa LRA,alipashwa kutia saini mkataba wa amani na serikali jana alhamisi jambo ambalo alikuwa alifanye wiki iliopita. Hata hivyo hakufanya hivyo akisema kuwa anataka kwanza kuelimishwa kuhusu masuala mawili.

Kwanza mustakbala wake kuhusiana na mahakama za kijadi za kwao zinazojulikana kama Mato Put.Na pia kuhusu sheria za Uganda ambazo zitashughulikia kesi za uhailifu baada ya kutiwa saini.

Hali hiyo ilileta wasiwasi kuwa huenda Kony asitie saini mkataba huo.Lakini aliahidi kuwa huenda leo Ijumaa au kesho jumamosi ndipo atatia saini mkataba huo.

Taarifa kutoka Ri Kwangba mpakani mwa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zinasema kuwa wajumbe wa serikali y Uganda,na wajumbe kutoka Umoja wa mataifa pamoja na waandishi habari waliokwenda huko kushuhudia sherehe hiyo ya kihistoria walilala huko wakisubiri kuona ikiwa leoIjumaa lililowapeleka huko litatekelezwa. Akiwa Nabanga mwa wandishi habari Mereike Schomerus anasema kuwa hali kwa sasa haileweki kwani hawajui kipi kinachoendelea.

Hali ilizidi kuwa ngumu kueleweka kufutia kujiuzulu kwa aliekuwa mkuu wa ujumbe wa LRA katika mazungumzo ya mani na serikali ya mjini Juba kusini mwa Sudan Dr.David Nyakorach Matsanga akisema kuwa ameshindwa kuwasilaina na Joseph Kony.

Na habari zaidi kutoka huko zinasema kuwa ujumbe wa serikali ya Uganda, ukiongozwa na waziri wa mambo ya ndani,Dr. Ruhakana Rugunda umondoka kutoka maeneo hayo na haijulikanai ikiwa umerejea Juba ama Kampala.