1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa amani kati ya serikali ya Kinshasa na makundi ya waasi Mashariki mwa Congo

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cvwl

GOMA:

Mkataba wa amani katika eneo la mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo untarajiwa kutiwa saini hii leo.

Wapatanishi katika mkutano wa amani unaofanyika Goma wanasema kuwa kuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Kinshasa na kiongozi wa kundi kubwa la waasi ,Generali Laurent Nkunda.

Makubaliano hayo ya jana yana nia ya kumaliza vita vya miezi kadhaa huko mashariki mwa Kongo ambavyo vimewalazimisha watu zaidi ya laki nne Unusu kuyakimbia makazi yao huko Goma.

Mazungumzo hayo yalianza kiasi cha wiki mbili zilizopita yanaudhuriwa na wawakilishi wa serikali,pamoja na zaidi ya vikundi 20 vya waasi na yanafadhiliwa na Umoja wa Ulaya,Umoja wa afrika pamoja na Marekani.