1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa azuru Kongo

Josephat Nyiro Charo12 Aprili 2010

Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na visa vya ubakaji na ukiukaji wa haki za binadamu kwenye maeneo ya migogoro, Margot Wallstrom, ameanza ziara ya siku nne Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

https://p.dw.com/p/MugV
Margot WallstroemPicha: AP

Bibi Wallstrom anatarajiwa kukutana badaye leo na waziri mkuu wa Kongo, Adolphe Muzito, na wanachama wengine wa serikali yake, na vile vile mashirika ya kiraia na yale yasiyo ya kiserikali ili kutathmini kwa pamoja kuhusu visa vya ubakaji dhidi ya wanawake na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu nchini DRC. Ziara hiyo itampeleka pia kwenye majimbo ya kivu ya kusini na ya kaskazini.

Mtayarishaji: Josephat Charo

Mhariri: Othman Miraji