1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

080710 D Guantanamo Aufnahme

Sekione Kitojo8 Julai 2010

Ujerumani inataka kuwachukua wafungwa wawili wa jela ya Guantanamo. Amesema hayo waziri wa mambo ya ndani Thomas de Meiziere jana mjini Berlin. Hatua hiyo imezua mjadala mkubwa mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/OEH4
Wafungwa wa jela ya Guantanamo kutoka kabila la Waigua kutoka China ambao wameonekana kutokuwa na makosa, lakini wameshindwa kupata nchi ya kuwapeleka kuishi, na hawawezi kurejea nyumbani nchini China.Picha: AP

Ujerumani  inataka  kuwachukua  wafungwa  wawili  wa jela  ya  Guantanamo. Amesema  hayo  waziri  wa  mambo ya  ndani  Thomas de Meiziere  jana  Jumatano  mjini Berlin. Uamuzi  huo  umeleta  mjadala  mkubwa  mjini Berlin.

Shirika  la  kutetea  haki  za  binadamu  Amnesty International  na  lile  la  Human Rights  Watch yameukaribisha  uamuzi  huo  wa  waziri  wa  mambo  ya ndani. Na  pia  upande  wa  upinzani  unaunga  mkono uamuzi  huo  wa   waziri  Thomas de Maiziere,   wa kuwachukua  wafungwa  hao  wawili  kutoka  jela  ya Guantanamo  nchini  Ujerumani. Dieter  Wiefelspütz  ni mtaalamu   wa  mambo  ya  ndani   kutoka   chama  kikuu cha  upinzani  cha  SPD.

Waziri  wa  mambo  ya  ndani  wa  serikali  ya  Ujerumani alichofanya  ni  sahihi  na  kinachongia  akilini.  Kwa kutumia  sheria  ameweza  kufanya  kile  ambacho marafiki  zake  katika  chama  wamekuwa  wakikizuwia, na hapa  nampongeza.

Hata  chama  cha  kijani, The  Greens  kimekuwa  mstari wa  mbele    katika  kupigania   kuwachukua  wafungwa  wa Guantanamo. Hata   hivyo   kiongozi  wa   kundi  la wabunge  wa  chama  hicho  katika  bunge  la  Ujerumani Volker Beck  hakumsifu  waziri  huyo  wa  mambo  ya ndani.

Uamuzi   huo  unakuja  wakati  muda  umepita  sana  na amechukua  tahadhari  sana.  Ujerumani  ingeweza  hapa kujishughulisha  zaidi.

Mtangulizi  wa  De Maizieres , Schäuble  amekuwa akisitisha  mara  kwa  mara  upokeaji  wa   wafungwa  hao kutoka  Guantanamo. Majimbo  kadha  ya  Ujerumani yamekuwa  yakikataa  kuwachukua  wafungwa  hao. Ukosoaji  dhidi  ya  mipango   hiyo  ulitokea  katika  miezi ya  hivi  karibuni  hususan   kutoka  chama  cha  CDU  na CSU. Waziri  wa  mambo  ya  ndani  wa   Bayern Joachim Herrmann  anatanabahisha   kuwa  uamuzi  huo  una  hali ya  kuuma  meno.

Suala  la  Guantanamo  linaweza  kujadiliwa  kisheria. Ndio sababu  wafungwa  hao,  kuwa  huko  sio  jambo  la  hatari. Mwenye  jukumu  na  jela  ya  Guantanamo  ni  Marekani na  sio  sisi   Ujerumani.

Wafungwa  wote  hao  wawili  watapelekwa  katika majimbo  ya  Rheinland Pfalz  na  Hamburg. Waziri  wa mambo  ya  ndani  wa  jimbo  la  Rheinland Pfalz  Karl-Peter  Bruch , anadai   kuwa  jimbo  lake  lilikuwa  makao ya  jeshi  la  Marekani  na  linawajibu  maalum  kwa Marekani . Julia Klöckner  ni  kiongozi  wa  CDU  na kiongozi  wa  upinzani  katika  jimbo  hilo.

Mimi  binafsi  siungi  mkono  mtazamo  wa  Bwana  Bruch, ambaye  ametoa  ombi  hilo  kwa  waziri  wa  mambo  ya ndani  ya  serikali  ya  shirikisho, kwamba  atamchukua mfungwa  mmoja  wa  jela  ya  Guatanamo. Lakini  ndio sababu   hivi  sasa  ni  muhimu  kuangalia  kwa  dhati matatizo  ya  wananchi  wa  jimbo  hili  na  kuangalia usalama  wao.

Waziri  wa  mambo  ya  ndani  wa  serikali  ya  Ujerumani anahakika, kwamba  wafungwa  wote  hao  wawili hawataleta  kitisho. Pamoja  na   hayo  wote  wawili wataendelea  kufuatiliwa. Kwa  vyovyote  vile  Ujerumani inataka  kuchukua  wafungwa  wengine  zaidi.  Kwa  hivi sasa   katika  jela  hiyo  ya  Guantanamo  kuna  wafungwa wapatao  180.

Mwandishi  :  Bölinger, Mathias/ ZR /  Sekione  Kitojo.

Mhariri :  Mohammed  Abdul Rahman

E N D E