Mjadala wa Kosovo waendelea. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mjadala wa Kosovo waendelea.

New York.

Maafisa wa Serbia na Kosovo wanaendelea kuvutana katika baraza la usalama la umoja wa mataifa leo, wakati Wakosovo wakidai uhuru haraka kwa jimbo lao na Waserbia wakidai kuwa jimbo hilo libaki kuwa sehemu ya ardhi yake. Pande zote mbili zina waungaji mkono katika baraza la usalama la umoja wa mataifa, Marekani pamoja na mataifa muhimu katika umoja wa Ulaya wakiunga mkono wito wa Kosovo wa kupatiwa uhuru na Urusi ikiunga mkono washirika wake Serbia na kutoa wito wa kuwa na majadiliano zaidi. Kikao hicho cha baraza la usalama kitalenga kuhusu ripoti iliyoandaliwa na wajumbe wapatanishi kutoka Marekani, umoja wa Ulaya na Urusi katika mazungumzo yaliyochukua miaka miwili baina ya Belgrade na Kosovo katika kutatua hali ya baadaye ya jimbo hilo la Kosovo. Mazungumzo hayo yalimalizika mwezi wa Novemba bila kupatikana makubaliano. Hashim Thaci , waziri mkuu mteule wa jimbo la Kosovo amewaambia waandishi wa habari kuwa Kosovo iko tayari kwa uhuru.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com