1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mivutano ya kibiashara kutawala mkutano wa G7

Bruce Amani
7 Juni 2018

Viongozi wa Kundi la nchi saba zilizostawi zaidi kiviwanda la G7 wanajiandaa kwa mkutano wa kilele unaoanza Kesho Ijumaa nchini Canada, na mazungumzo hayo yanatarajiwa kuwa makali kutokana na misimamo ya Trump

https://p.dw.com/p/2z4Rp
Japan Flaggen der G7-Mitgliedsstaaten 2016
Picha: picture-alliance/dpa/K. Ota

 huku mazungumzo hayo yakitarajiwa kuwa makali kuhusiana na misimamo ya Donald Trump kuhusiana na sera zake za biashara. 

Mkutano wa kilele wa G7, ambao utawaleta pamoja viongozi wa Canada, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan, unakuja katika wakati ambapo wengi wanauona kuwa ni wakati wa kushuhudia mgawanyiko wa kihistoria kati ya Marekani na washirika wake wakuu wa Amerika Kaskazini, Ulaya na Asia.

Siku chache zilizopita, utawala wa Trump ulitangaza kiwango kikubwa cha ushuru kwenye bidhaa za chuma cha pua na bati zinazoingizwa Marekani kutoka washirika watano kati ya sita wa G7. Pia ulianzisha hivi karibuni uchunguzi wa kibiashara ambao huenda ukasababisha kutangazwa ushuru zaidi kwa magari yanayoingizwa Marekani.

Ushuru huo unatokana na kile kinachoonekana kuwa ni sababu za uwongo, kwamba bidhaa zinazoingizwa nchini humo ni kitisho kwa usalama wa Marekani, licha ya ukweli kwamba nchi zote zitakazokuwa katika mkutano wa G7 ni wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO pamoja na Marekani au zina ushirikiano wa muda mrefu wa usalama na Marekani kama vile Japan.

Wakati viwango hivyo vya ushuru, ambavyo Ulaya na Canada zimepambana kutaka viondolewe, ndiyo vya karibuni, ni vya mwisho tu kati ya orodha inayoendelea kuwa ndefu ya tofauti zinazoibuka kati ya Marekani na washirika wake.

Deutschland Bundestag Regierungsbefragung | Angela Merkel und Beatrix von Storch
Merkel anataraji mazungumzo ya G7 kuwa magumuPicha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Kabla ya hatua ya kutangaza kodi hizo mpya, utawala wa Trump - tena kinyume na washirika wake - ulijiondoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran. Na katika hatua yake ya awali ambayo iliharibu mahusiano na washirika wake, Trump aliiondoa Marekani katika mkataba wa tabianchi wa Paris baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika mkutano wa G7 mwaka jana nchini Italia.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Canada Justine Trudeau wote hivi karibuni walishindwa kumshawishi Trump kutoweka ushuru huo dhidi ya washirika wake. Daniel Price, aliyekuwa mwakilishi wa kibinafsi wa George W. Bush katika mikutano ya kilele ya G8 na G20, anasema maamuzi hayo ya upande mmoja yanayochukuliwa na Trump dhidi ya washirika wake yanahirubu mahusiano

Kwa upande wa Roland Paris, mshauri mkuu wa zamani wa sera za kigeni wa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, ambaye sasa ni profesa wa masuala ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ottawa, anasema migawanyiko ya sasa kati ya Marekani na Canada ni mikubwa zaidi kuliko mingine yoyote ya awali kati ya nchi hizo jirani

Licha ya msuguano kati ya Marekani na washirika wake, ambayo Price na Paris hawaamini kuwa yatatatuliwa, wanahisi kuwa mkutano wa G7 unaweza bado kuwa muhimu - kwa ajili ya kuelezea tu tofauti zao kati ya pande hizo. Aidha washauri hao wakuu wa zamani wanasema kuwa hakutakuwa na matokeo yoyote makubwa yatakayopatikana kwenye mkutano huo, kwa mfano kuhusu biashara.

Mwandishi:Michael Knigge
Tafsiri: Bruce Amani
Mhariri: Iddi Ssessanga