1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mitetemeko imezusha hofu ya Tsunami

P.Martin15 Septemba 2007

Mitetemeko ya ardhi iliyofululiza katika kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia, imesababisha hali ya hofu katika eneo hilo la Asia.

https://p.dw.com/p/CB1E
Ufa kwenye barabara ya Bengkulu,kisiwani Sumatra baada ya tetemeko kubwa la ardhi
Ufa kwenye barabara ya Bengkulu,kisiwani Sumatra baada ya tetemeko kubwa la ardhiPicha: picture-alliance/ dpa

Wasaidizi nchini Indonesia,wanaharakisha kupeleka misaada sehemu mbali mbali za Sumatra,baada ya mfululizo wa mitetemeko ya ardhi juma hili kuuwa hadi watu 17 na kuteketeza maelfu ya nyumba.Wakuu wa misaada wamesema,chakula na misaada mingine imefika katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika. Hata hivyo,bado kuna watu wengi wanaolala nje kwa sababu ya uhaba wa mahema.

Wataalamu wanahofia kuwa tena,huenda kukatokea gharika la Tsunami kama mwaka 2004.Wakati huo, zaidi ya watu 230,000 walipoteza maisha yao katika nchi za eneo la Asia.