1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misukosuko katika masoko ya hisa Marekani, Ulaya na Asia

9 Agosti 2011

Thamani katika masoko ya hisa ya Ulaya zimeporomoka kwa mara nyengine tena hii leo, zikishawishiwa na hali namna ilivyo katika masoko ya hisa barani Asia na katika masoko ya hisa ya Marekani huko Wallstreet.

https://p.dw.com/p/12DOL
Thamani katika masoko ya hisa imeporomokaPicha: Fotolia/Dan Race

Baadhi ya wadadisi na wakuu wa mashirika ya fedha wanaamini hata hivyo thamani katika masoko ya hisa hazitakawia kuanza kujirekebisha na kupanda.

"Kiwango cha malipo ziada ya kinga ya muda mrefu ni hatari zaidi kuliko kuzorota uchumi kwa sababu kinafikiwa kiwango sawa na kile kilichowahi kutokea mapema miaka ya 80 pamoja na kudorora mara dufu uchumi wa Marekani," amesema Benoit Peloille -mtaalam wa kiuchumi katika shirika la hisa la Natixis.

Saa nne na dakika kumi thamani ya hisa za shirika la CAC 40 mjini Paris iliporomoka kwa asili mia 1.29 baada ya kuteremka hapo awali hadi pointi 3.043,24. Mdadisi wa masuala ya kiuchumi kutoka shirika la Aurel-BGS anaamini kiwango hicho kitafikia pointi 2.960 hivi karibuni.

Katika masoko mengine ya hisa hali ni sawa na hiyo,London imepoteza asili mia 2.26 na Frankfurt asili mia 1.84.

Börsen reagieren
Soko la hisa nchini AustraliaPicha: picture alliance/dpa

Thamani ya mafuta imepungua kwa dola mbili kila pipa.Bei ya mafuta ghafi na mepesi ya Marekani imeporomoka kwa asili mia 2.9 na kufikia dola 78.90 kwa kila pipa moja na Brent ya Uingereza imepungua kwa asili mia 2 na kukarubia dala mia moja kwa pipa.

Wasi wasi umetanda na masikio yanategwa Marekani ambako matokeo ya shughuli za kiuchumi za makampuni matatu kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo mchana. Wadadisi wanahofia uchumi wa Marekani usije ukazidi kuathirika ikiwa matokeo hayo hayatakuwa mazuri.

Licha ya hofu zilizoko rais Barack Obama anasema:

"Thamani katika masoko ya hisa zinaweza kupanda na kuporomoka. Hivyo ndivyo Marekani ilivyo. Bila kujali nini wakala zinazopima nguvu za kifedha zisemavyo: Sisi daima ni nchi ya A tatu."

Frankfurt Börse Crash Kursverluste Finanzkrise Jean-Claude Trichet
Mwenyekiti wa benki kuu ya Ulaya Jean-Claude TrichetPicha: dapd

Katika zoni ya Euro benki kuu ya Ulaya ilizidisha hofu jana kwa kununua dhamana za mikopo za Italia na Hispania. Kwa mujibu wa uchunguzi uliosimamiwa na shirika la habari la Reuters katika mashirika makubwa makubwa ya kiuchumi, benki kuu ya Ulaya ingebidi inunue thamani za Italia na Hispania kwa angalao Euro bilioni 100 ili kuweza kuiokoa zoni ya Euro toka migogoro.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters

Mhariri: Josephat Charo