Miripuko yatikisa Msikiti Mwekundu | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Miripuko yatikisa Msikiti Mwekundu

Nchini Pakistan,hii leo vikosi vya usalama na wanamgambo waliojificha ndani ya Msikiti Mwekundu walifyatuliana risasi katika mji wa Islamabad.

Ukuta wa Msikiti Mwekundu mjini Islamabad ukiwa na alama za risasi

Ukuta wa Msikiti Mwekundu mjini Islamabad ukiwa na alama za risasi

Hapo awali,miripuko miwili iliutikisa msikiti huo huku vikosi vya usalama vikizidi kuwazingira wale waliojificha ndani ya msikiti.Maalim mmojawapo amesema,yeye na wafuasi wake wapo tayari kufa badala ya kusalim amri.

Inasemekana kuwa katika jengo hilo,kuna kama watu 300 ikiwa ni mchanganyiko wa wanaume,wanawake na watoto. Wakati huo huo,mashhehe wengine hii leo wanatazamia kuzungumza na maalim huyo,ili watoto walio katika msikiti huo wapate kuachiliwa huru.

Hadi hivi sasa watu 19 wameuawa katika mapigano yaliyozuka kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo waliojificha nsikitini.Viongozi wa Msikiti Mwekundu wanataka sheria kali za Kiislamu zitumike kote nchini Pakistan.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com