1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Milipuko ya mabomu na risasi vyaitingisha Nigeria

5 Novemba 2011

Milipuko mitatu tofauti ya mabomu ya kujitoa mhanga imetokea kwenye makao makuu ya jeshi katika mji wa Maiduguri na minginge ya mabomu ya kutegwa barabarani imelitikisa eneo la kaskazini mwa Nigeria ijumaa iliyopita.

https://p.dw.com/p/135VZ
Gari lililoripuliwa MaiduguriPicha: AP

Kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda na jeshi wamesema mashambulizi kadhaa ya mabomu na risasi yamefanyika katika maeneo ya miji mingine miwili ya magharibi.

Matukio hayo, yanayodaiwa kufanya na kundi la waislam wenye itikadi kali la Boko Haram yametajwa kuwa makubwa sana kutokea katika siku za hivi karibuni.

Kundi hilo limekuwa likifanya maangamizi dhidi ya viongozi wa eneo hilo kame lililopo kas/mash mwa jimbo la Berno.

Karte Nigeria mit Bundesstaat Borno und der Stadt Maiduguri
Ramani ya Nigeria ikionesha eneo la Maiduguri

Luteni Kanali Hassan Mohammed, kamanda wa kikosi kazi katika kukabiliana na uhalifu katika eneo hilo alisema mwanjeshi mmoja na raia sita wamejeruhiwa.

Awali milipuko mingine mitatu ya mabomu yaliotegwa barabarani ililipuka katika maeneo tofauti sambamba na mashambulio yaliyopangwa.

Milipuko hiyo imetokea katika kata za Maiduguri, Jajeri na chuo cha kiislamu cha El-kanemi, matukio yote yametokea muda wa sala ya ijumaa na kuwafanya waumini waliokuwa misikitini kukimbia.

Milipuko hiyo ya kila siku katika maeneo ya kask/mash inayofanyika sambamba na matukio ya ufyatulianaji risasi inadaiwa kufanywa na kundi linaloitwa Boko Haram.

Boko Haram, kundi la kiislamu lenye itikadi kali, jina lake lina maana ya "Elimu ya magharibi marufuku". kwa kwaida mashambulizi hayo yanalenga maeneo ya umma, viongozi wa kidini.

Katika shambulio lililofanyika katika makao makuu ya kijeshi imethibitika kwamba mtu aliejitoa mhanga anatoka katika kundi la Boko Haram.

Uchunguzi unaeleza kwamba namna ya shambulio hilo lilivyofanyika inajidhihirisha wazi kwamba mbinu iliyotumika imerudiwa kwa mara ya pili.

Tukio lingine kama hilo lilifanyika katika makao makuu ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Abuja na kusababisha vifo vya watu 26 nchini humo.

Boko Haram wanasema wanataka sheria za kiislamu zitumike nchini Nigeria. Kundi hilo linaungwa mkono na vijana wengi wa wasio na ajira katika maeneo ya vijijini.

Kundi hilo limeendelea kukuwa taratibu huku wachambuzi wa mambo wakisema lina mfungamano na kundi kubwa la al-Qaeda la kaskazini mwa Afrika.

Hata hivyo viongozi katika maeneo yaliyotokea matukio hayo wanasema bado haijawa wazi kama kuna vifo vilivyotokea kutokana na milipuko ya mitatu ya mabomu katika mji wa Maiduguri.

Katika muendelezo wa tukio kama hilo mtu anaehisiwa kuwa ni kutoka kundi la Boko Haram alishambulia miji ya Damaturu na Potiskum iliyopo umbali wa kilometa 100 magharibi mwa Maiduguri katika jimbo la Yobe.

Mashuhuda wanasema mtu huyo alifyatuliana risasi na vikosi vya usalama.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR
Mhariri: Sekione Kitojo