1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Migomo yaanza kuleta athari Ufaransa

Sekione Kitojo16 Oktoba 2010

Migomo dhidi ya mpango wa pensheni wa rais Nicolas sarkozy yaanza kuleta athari, ambapo viwanja vya ndege vinakosa mafuta.

https://p.dw.com/p/Pffn
Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa.Picha: AP

Ufaransa  inakabiliwa  na  ishara  za  kwanza  za  uhaba wa  mafuta  wakati  migomo  dhidi  ya   mageuzi  ya  Rais Nicolas  Sarkozy   ya  pensheni   ukiingia  katika   siku yake  ya  nne. Mgomo  katika   kiwanda  cha  kusafisha mafuta  ambayo  hutumika  katika  viwanja  vya  ndege , umesababisha  mafuta  kutofika  katika  viwanja  hivyo kupitia  bomba  la  mafuta  liendalo  katika   viwanja  vikuu viwili  vya  ndege  mjini  Paris  tangu  jana  Ijumaa.

Kampuni  ambayo  inasafirisha   mafuta  kupitia  bomba hilo  imesema   kuwa   uwanja  mkuu  wa  ndege  katika mji  wa  Paris , Charles de Gaulle, unaweza  kukosa mafuta  ifikapo  mapema  wiki  ijayo. Wakati  huo  huo, Rais  Sarkozy  ametuma   kikosi  cha  polisi  wa  kuzuwia ghasia   ili  kumaliza  uzuwiaji  huo  wa  huduma  ya mafuta  katika  viwanda  12  vya  kusafisha  mafuta  nchini humo. Vyama  vya   wafanyakazi  nchini  Ufaransa vinapinga  mipango  ya  serikali  ya  kuongeza  umri   wa kustaafu.