1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo mwishoni mwa wiki

1 Septemba 2008

Bayern Munich yajipatia ushindi wake wa kwanza msimu mpya wa Bundesliga.

https://p.dw.com/p/F8fl
Munich (nyekundu)Picha: AP

Ligi mashuhuri za Ulaya zimerudi uwanjani,lakini Real Madrid na FC Barcelona za Spain, hazikuanza vyema.

Bayern Munich -mabingwa wa Ujerumani wakiongozwa na kocha wao mpya Jurgen klinsmann, wajipatia ushindi wao wa kwanza tangu kuanza msimu.

Taifa Stars ya Tanzania yaondoka kesho kuelekea Mauritius kabla kukumbana na Sudan.

Tukianza na Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,mabingwa Bayern Munich walimpatia jana ushindi wake wa kwanza kocha wao mpya Jurgen Klinsmann walipoichapa Hertha Berlin mabao 4:1 la kufuta machozi.

Mshambulizi wao hatari mtaliana Luca Toni ndie alielifumania kwanza lango la Berlin mnamo dakika ya 12 ya mchezo.Baadae mlinzi Philipp Lahm na Bastian Schweinsteiger wakaongeza mabao 2 ya mikwaju ya penalty.

Shangwe kubwa lakini uwsnajani zilisikika pale mshambulizo wao mwengine Miroslav kloser alipokata kiu kirefu cha kutotia bao alipotia bao pia la mkwaju wa penalty dakika 20 kabla firimbi ya mwisho.

Baadae Miroslav klose,alieibuka mtiaji mabao mengi katika kombe lililopita la dunia,alisema:

"Meneja alikuwa wakati wote nyuma yangu na kila wakati akinambia maneno muwafaka.Kwani, wanaona ninajitahidi ili kufanikiwa na mwishoe,hii imezaa matunda."

Bao hilo la klose, linatazamiwa sasa kukomesha maneno mengi kwanini Klose hatii tena mabao.Alitia bao 1 tu mwaka huu wa 2008 kabla la jana.ilikua msimu uliopita hapo Machi.

Ushindi wa jana wa kwanza kwa mabingwa Bayern munich uliweka nafasi ya 7 katika orodha ya Ligi ikiwa na pointi 5 kutoka mevhi 3.Stuttgart ikaizaba jana Hannover 2:0 kufuatia mabao ya Mario Gomez na Pavel Pardo.Schalke

04 iliparamia kileleni mwa Bundesliga kutokana na tofauti ya magoli na Hamburg iliotimua ilioizaba Bielefeld mabao 4-2.Schalke ilitamba kwa bao 1:0 mbele ya Bochum.

Borussia Dortmund iliitoa Cottbus kwa bao 1:0.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza,changamoto kati ya Mabingwa Manchester united na Fulham iliahirishwa hapo mwishoni mwa wiki,lakini mahasimu wao chelsea walipoteza pointi 2 za kwanza msimu huu walipomudu suluhu tu ya bao 1:1 na Tottenham hotspur.Arsenal iliikandika Newcastle united mabao 3:0 .Bolton Wonderers walitoka bila kwa bila na West Bromwich Albion huku West Ham united wakiikomea pia Blackburn Rovers mabao 3:1.Portsmouth ikaikandika Everton mabao 3:0.Wigan Athletic ilijaza kikapu cha Hull City kwa mabao 5:0 wakati middlesbrough ilitamba kwa 2:1 kati yake na Stoke City.

Chelsea hatahivyo inaoongoza orodha ya Ligi kwa pointi 7 ikifuatwa na Liverpool pia point 7.

Manchester united ambayo haikucheza mwishoni mwa wiki ina pointi 4.

Tugeukie sasa La Liga-ligi ya Spian:

Mabingwa Real Madrid na mahasimu wao FC Barcelona wote wawili hawakuanza uzuri mwishoni mwa wiki.Timu zote mbili jana zilishindwa: Real ilikandikwa mabao 2:1 na Deportivo La Coruna na hilo ni pigo lao la sita kutoka kwa La Coruna.

FC Barcelona nayo ikazabwsa bao 1:0 na Numancia, timu iliopanda msimu huu daraja ya kwanza ya La Liga.

Leo, Real madrid inatazamiwa kufanya jaribio la mwisho la kumuajiri mtiaji mabao mengi katika kombe la ulaya mwaka huu-David villa kutoka Valencia.

Katika Serie A au ligi ya Itali, mashabiki 7 walitiwa mbaroni baada ya kuzuka machafuko mwanzoni tu mwa msimu mpya.

Mashabiki 4 walikuwa wa Napoli na 3 wa AS roma.Garimoshi liliharibiwa na kiasi cha mashabiki 1000 wengi wao wakiwa hawana tiketi wakipanda traain hiyo kuelekea uwanjani Roma.

Wakati wa safari hiyo, wahuni hao walivunja madirisha na vyoo vya train hiyo na kusababisha hasara ya euro laki 5.

Mpambano kati ya roma na Napoli lakini ulimalizika suluhu bao 1:1.Mabingwa AC milan wakicheza na stadi wao mpya Ronaldinho, walizabwa bao 2:1 na

Bologne.Inter Milan ilitoka suluhu bao 1:1 na Sampdoria.

Ingawa Taifa Stars, Tanzania haina matumaini tena ya kukata tiketi ya kombe lijalo la dunia,inafunga safari kesho kwenda Mauritius ikitumai alao kufuta machozi na kuaga kwa heshima kama mwanamichezo wetu George Njongopa anavyosimulia kutoka Dar-es-salaam:

Michezo ya olimpik ya walemavu itaanza mwishoni mwa wiki hii ijayo

mjini Beijing-wiki 2 tangu kumalizika rasmi ile ya 29 ya majira ya kiangazi ya wanariadha wasio-walemavu.

Wanariadha wa kiafrika wanatazamia pia kutia fora katika michezo hii.Australia iliaga kikosi chake hii leo kilichoondoka Sydney, ikitumai wanariadha wake walemavu watarejea na medali hadi kufikia 1000 kwa Australia tangu michezo hii kuanza 1960.Wanariadha-walemavu wa Australia wameshashinda hadi medali 908 tangu michezo hii kuanzishwa miaka 48 iliopita mjini Roma.

Iwapo itajaza pengo hilo lililobaki na kufikia medali 1000 huko Beijing,yafaa kusubiri kuona.

Wenyeji china, wamejiwinda nao kuwaigiza wenazo-wasio walemavu walinyakua medali 51 za dhahabu na kuparamia ngazi ya medali kileleni.

Na kwa taarifa hiyo ya kufungua pazia kwa michezo ya Olimpik ya walemavu inayoanza Beijing jumamosi ijayo, ndio sina budi bali kuishia hapo kwa leo.