1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIAMI:Wakimbizi 22 wa Haiti waliwa na Papa

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4W

Kiasi cha wakimbizi 22 wa Haiti wamekufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria wakijaribu kuingia Marekani, kuzama katika eneo lenye papa wengi.

Boti hiyo ilikuwa na watu wapatao 150, ambapo 73 waliokolewa na wengine 50 hawajulikani waliyopo.

Walinzi wa pwani yaMarekani wamesema kuwa waliona miili kadhaa ikielea mingi ikionekana imeliwa na papa.