1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIAMI: Kimbunga kinaelekea Ghuba ya Mexiico

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBY8

Kimbunga kilichopewa jina “DEAN“ kimezidi nguvu baada ya kusababisha hasara kubwa kisiwani St.Lucia kwenye Bahari ya Karibean.Kituo cha Kitaifa cha Kutabiri Vimbunga,kilicho na makao yake Miami nchini Marekani,kimearifu kuwa kimbunga “DEAN“ sasa kinaelekea Jamaika na Ghuba ya Mexico kwa mwendo wa zaidi ya kilomita 208 kwa saa.Watabiri hali ya hewa wanasema,kimbunga hicho kinatazamiwa kufika Ghuba ya Mexico kwenye visima vya mafuta na gesi katikati ya juma lijalo.