1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka mitano tangu majeshi ya Marekani kuuteka mji wa Baghdad

Kalyango Siraj9 Aprili 2008

Watu 16 wauwa na wengine kujeruhiwa katika ghasia Baghdad

https://p.dw.com/p/Df4i
Mwanajeshi wa Iraq akishiongoza magari katika barabara za mjini Baghdad.Miaka mitano baadae baado ghasia na mauaji yanaendelea katika mji huo.Picha: AP

Watu 16 wameuawa leo jumatano katika mtaa wa Washia wa jiji la Baghdad nchini Iraq wakati wa mapigano kati ya vikosi vya usalama dhidi ya wanamgambo wa Kishia ikiwa imetimia miaka mitano mji huo kuanguka katika mikono ya majeshi ya Marekani kutoka mikononi ya utawala wa Saddam Hussein.

Leo jumatano ikiwa ndio imetimia miaka mitano tangu majeshi ya Marekani kuuteka mji wa mkuu wa Iraq Baghdad lakini baado vifo na uhalifu vinaendelea katika mji huo.

Mbali na waliouawa katika kiunga cha Sadr City,ambacho kiko chini ya amri ya kutotoka nje kutokana na ghasia,lakini pia eneo ambalo linalindwa sana la Green Zone nalo limeshambuliwa kwa mizinga.Hata hivyo hakujatolewa taarifa za majeruhi.

Eneo hili la Green Zone ndiko kunapatikana majengo ya serikali balozi za Marekani na Uingereza pamoja na mashirika muhimu ya kigeni.

Polisi mjini Baghdad inasema kuwa miongoni mwa waliouawa katika Sadr City ni watoto watatu baada ya nyumba walimokuwa kuangukiwa na kombora lililovurumishwa.Kiunga hicho ndiko kunapatikana wapiganaji wa Kishia wa jeshi la Mahdi ambalo ni tiifu kwa kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali Muqtada al-Sadr.

Tena katika tukio jingine leo jumatano,kombora moja pia lilianguka katika eneo wanakokaa raia wa kawaida saa za mchana. Kombora hilo limewauwa watu saba na kuwajeruhi wengine 36 kwa mujibu wa polisi na maafisa wa utibabu.

Ghasia yaonekana zinaendelea.Mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Iraq Generali David Petraeus ameliambia baraza la Congress la Marekani jumanne kuwa viwango vya ghasia pamoja na vifo vya raia wa kawaida vimepungua tangu Septemba.Aidha ametaka makamanda waandamizi kutafakari hali ya sasa nchini Iraq.

Barabara nyingi mjini wa Baghdad zilikuwa tupu na kutokana na amri ya kutotoka nje ya siku moja wakati wa kuadhimisha miaka mitano tangu mji huo uanguke katika mikono ya askari wa Marekani.

Ulinzi uliimarishwa,maduka na maghala kadhaa yalifungwa na ofisi za serikali hazikufunguliwa na pia magazeti hayakuonekana kando mwa barabara kinyume na kawaida.

Licha ya waShia kupata maendeleo ya kisiasa tangu majeshi ya Marekani yaingie katika mji huo Aprili 9 mwaka wa 2003,baadhi yao sanasana wanaokaa katika sehemu ya Sadr City wanasema majeshi ya Marekani ni lazima yaondolewe kutoka nchini humo.

Muqtada al-Sadr alikuwa ametangaza maandamano ya mamilioni ya watu leo ktika mji huo dhidi ya Marekani lakini amri ya kutotoka nje imewazuia.

Habari zingine zinasema kuwa maandamano yalisitishwa baada ya kiongozi wa kidni kuwaambia wafuasi wake badala yake wajihami dhidi ya mauaji yanayoweza kutokea wakati wa kuadhimisha siku hii.

Idadi kamili ya raia waliouawa tangu mwaka wa 2003 ni vigumu kujulikna.Lakini baadhi ya mashirika yanayojihusisha na matukio nchini Iraq yanasema idadi ya watu hao ni takriban 90,000.

Wanajeshi wa Marekani waliofariki kufikia sasa wanafikia 4,000.Huku vita hivyo vikiwa vimeigharimu serikali ya Marekani $ 500 billioni.Wakimbizi wa Iraq wanafikia 2 millioni ,huku wengine 2 millioni wameachwa bia ya makazi.