1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 45 tangu kuuwawa mwanamapinduzi, Ernesto Che Guevara.

9 Oktoba 2007

Ernesto Che Guevara, rafiki wa chanda na pete wa kiongozi wa mapinduzi ya Cuba, Fidel Castro, katika msitu ya Bolivia, karibu na mji wa Higuera, kumelifanya jina la mpiganaji huyo wa chini kwa chini lisife.

https://p.dw.com/p/C7iJ
Mwanamapinduzi, Ernesto Che Guevara
Mwanamapinduzi, Ernesto Che GuevaraPicha: AP

Kuuliwa hapo Oktoba 9 mwaka 1967 kwa Akiwa pamoja na wapiganaji wenzake 17 waliochoka na kuvunjika moyo, Che Guevara alizungukwa na wanajeshi 650 wa Bolivia pamoja na makachero wa Shirika la Ujasusi la Kimarekani, CIA, akajeruhiwa kwa risasi, na maisha yake yakamalizwa kabisa kwa kufyetuliwa risasi tisa na luteni wa jeshi aliyelewa. Julia Cortez, mwalimu, alikuwa mtu wa mwisho kumuona Che bado yungali hai.

+ Naam alikuwa katika hali mbaya, kiafya, amekonda, nguo zinampwaya. Mtu aliona vibaya kumuona katika hali hiyo, Lakini mtu aliweza kumtambuwa kutokana na macho yake mazuri, mwili wake wote wa nje ulikuwa wa kuvutia.+

Watu wengi, hata wale ambao walikuwa bado hawajazaliwa wakati huo, wanalitukuza jina la Che Guevara na wanapata hisia ya kutaka kuendeleza yale aliyoyapigania. Waliomuuwa Che Guevara walitaka si tu mwili wake utoweke, lakini pia fikra zake, mtu aliyetambuliwa kuwa ni mpiganaji wa uhuru. Maiti ilioneshwa kwa watu na kuchomwa moto karibu na kiwanja kidogo cha ndege. Lakin kinyume na ilivofikiriwa, sura ya mwanamapinduzi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 39 pale alipouliwa, imebakia katika vichwa vya wapenzi na maadui zake.

Ali Sultan, aliyewahi kuwa waziri katika serekali ya mapinduzi ya Zanzibar, anamkumbuka Che Guevara kama hivi:

Insert: Ali Sultan 1 ….

Pale kila mwamko wa fikra za siasa za kijamaa unapopata nguvu katika Amerika ya Kati na Kusini, ndipo jina la Che Guevara linazdi kuheshimika. Wale watu ambao sasa wanapinga utanda wazi wanamtathmini Che kama mlezi wa fikra zao zenye kutetea maslahi ya walala hoi na wanaoonewa katika mabara yote ya dunia. Pia Che Guevara limekuwa kwa muda mrefu jina lenye kuvutia katika biashara ya mavazi, muziki wa aina ya Pop, matangazo mengine ya biashara na alama ya maisha mbadala.

Kama kamanda wa wapiganaji wa chini kwa chini huko Cuba, na ambayo mwaka 1959 yaliupinduwa utawala wa mdikteta Fulgigencio Batista, mzaliwa huyo wa Argentina, pamoja na Fidel Castro ndio waliokuwa bongo nyuma ya utawala mpya huko Havana. Che Guevara alikuwa hajashughulika kuwa na cheo katika utawala huo mpya, lakini mwaka 1965 aliondoka Cuba na kurejea katika mizizi ya harakati zake za kimapinduzi. Alijaribu kuziwasha cheche za mapinduzi huko Kongo na baadae Bolivia.

Katika nchi zote hizo mbili alishindwa. Huko Kongo alijaribu kuyasaidia majeshi ya waasi, chini ya marehemu Laurent Kabila, yaingie madarakani. Mbegu hizo za kimapinduzi alizotaka kuzipandisha Kongo, alifikiria zitatoa matunda yake kwa kufanyika mapinduzi katika bara zima la Afrika. Jee jaribio lake la Kongo lilishindwa? Ali Sultan, mtu aliyemjuwa vyema Che Guevara, anasema Hata kidogo:

Insert: Ali Sultan 2

Baadae alielekeza nguvu zake huko Amerika ya Kusini na akifikiria kwamba huko kutakuwa ni chimbuko la mapinduzi ya dunia. Aliitathmini vibaya hali ya kisiasa na ya kijamii katika Bolivia, watu wa asili katika maeneo hayo walimpa kisogo, huku jeshi la serekali pamoja na majasusi wa Kimarekani wakizifuata nyendo za mwanamapinduzi huyo .

Che Guevara alikuwa sio msuluhishi wa matatizo ya dunia hii, lakini alikuwa mwananadharia ambaye fikra na vitendo vyake, kupitia haki aliyoiamini ya kutumia nguvu na kuuwa, alitaka viamuwe mustakbali wa watu. Kikosi cha wauaji wa Kipalastina ambacho mwaka 1977 kiliiteka nyara ndege ya Shirika la Kijerumani la Lufthansa, ili kushikilia waachwe huru magaidi wa jeshi jekundi la Ujerumani, RAF, walivaa flana zenye picha ya Che Guevara. Washabiki wa Che Guevara walitamani ifike siku ambapo ustaarabu wa kisiasa waliouchukia na ambao hawawezi wala hawataki kuishi ndani yake utafutwa kabisa hapa duniani.

Vijana na wanafunzi wanaopinga amri zozote za kutoka juu wanamuona Che Guevara na kumtukuza kama mbadala wa uhuru. Tangu mwanzo alitaka kuweko udikteta safi wa chama kimoja katika Cuba, jambo ambalo bila ya kujali lilipelekea sauti yeyote ya upinzani kunyamazishwa.

Pale kiongozi wa Urussi, Nikita Kruschov, aliporegeza kamba kutokana na mbinyo wa Wamarekani na kukubali kuyaondosha maroketi ya kinyukliya ya masafa ya wastani ya nchi yake kutoka Cuba, Che Guevara alimlaani kiongozi huyo wa Urussi kwa kuuridhia ubeberu wa Marekani, na badala yake yeye alionyesha huruma yake kwa wakoministi wa Kichina.Pale mwaka 1965 alipoilaumu wazi wazi Urussi, Fidel Castro alikuwa hawezi tena kumstahamilia. Che aliondoka Cuba.

Baada ya kushinda mapinduzi ya kikominsti ya Cuba mwaka 1957, Che Guevara alichukuwa uongozi wa mahakama ya kimapinduzi ambayo iliwahukumu kwa haraka maelfu ya watu walioitwa wapinzani wa mapinduzi na mamia yao kupewa hukumu za vifo.

Ali Sultan, waziri wa zamani katika serekali ya mapinduzi ya Zanzibar, hakubali kwamba Che Guevara alikuw akatili mno kwa wapinzani wa mapinduzi ya Cuba:

Insert: Ali Sultan 3

Kama waziri wa viwanda, mwaka 1961 alianzisha mpango wa uchumi wa mpangilio na kulazimisha nchi hiyo ipige hatua za haraka kujenga viwanda na kuzidisha uzalishaji wa miwa inayotoa sukari. Aliupinga sana ubinafsi katika jamii ya Cuba.

Che Guevara alikuwa kama mwiba katika koo ya siasa ya nje ya Marekani. Tena Ali Sultan kutoka Zanziba:

Insert: Ali Sultan 4

Somo gani Waafrika wanajifunza kutokana na maisha ya mtu huyo, aliyesomea udaktari chuo kikuu, na mwishowe kuwa mwanamapinduzi na mopiganaji wa misituni. Ali Sultan, mtu aliyemuona uso kw amacho Che Guevara anasema:

Insert: Ali Sultan 5

Mwaka 1977, mabaki ya Ernesto Che Guevara yalichukuliwa kutoka Bolivia na kuzikwa Santa Clara, Cuba.