1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 20 tangu ukuta wa Berlin ulipoporomoshwa

Oumilkher Hamidou10 Novemba 2009

Maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa serikali kutoka nchi 30 za dunia wamehudhuria sherehe kubwa mjini Berlin

https://p.dw.com/p/KSul
Umati wa wajerumani wamesimama mbele ya lango la Brandenburger Tor mjini Berlin kuadhimisha miaka 20 ya kuporomoka ukutaPicha: AP

Sherehe za kusisimua za miaka 20 tangu ukuta wa Berlin ulipoporomoka zimekamilika katika mji mkuu wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani.Ilikua siku ya kumbukumbu,siku ya onyo na pia siku ya kutafakari:Hata hivyo November 9,siku ya kuporomoka ukuta ilisherehekewa kikamilifu.Maelfu ya watu na viongozi wa mataifa zaidi ya 30 wamehudhuria sherehe hizo kati kati ya mji mkuu Berlin.

Katika uwanja wa Pariser Platz karibu na lango la Brandenburger Tor mikururo ya watu wanaongozana.Kuna wanaosema idadi yao imepindukia watu laki moja.Mianvuli haikua na idadi mnamo siku hiyo iliyogubikwa na mvua.Kundi la wanamuziki wa serikali wakiongozwa na Daniel Barenboim ,wakiwa ndani ya banda kubwa jeupe limekua likiwatumbuiza watu-Miongoni mwao wameketi viongozi kadhaa wa serikali za kigeni.Kundi hilo la wanamuziki limeanza kuwatumbuiza watu kwa kipande cha muziki cha Richard Wagner.

Uwanjani kila mmoja anasikiliza kwa makini bila ya kujali hali ya mbaya ya hewa iliyokuwepo.Wengi wametokea mbali hadi kufika Berlin -walitaka na wao pia kusherehekea moja kwa moja miaka 20 ya kuporomoka ukuta .

"Tulitaka na sisi pia kushiriki,seuze tena ukuta ulipoporomoka tulikua bado wadogo."

Kumechangamka kweli kweli.Kupata fursa ya kujionea tena yaliyotokea miaka 20-wakati ule tulisikia kama ukuta umeporomoka,na leo tunajionea wenyewe jinsi mambo yalivyo."

Mambo bambam,super,watu wanasukumana kuweza kuingia katika uwanja wa sherehe-miaka inapita haraka kweli kweli.."

Baadae ikawa zamu ya wageni wa heshima kukamata kikuza sauti na kuonyesha furaha yao kuweza kuwa miongoni mwa wanaosherehekea siku hii ya November tisaa.

Hillary Clinton bei Feier am Brandenburger Tor Berlin
Waziri wa nje wa Marekani akihutubia katika sherehe za miaka 20 ya kuporomoka ukuta katika uwanja wa Brandenburger TorPicha: AP

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton anasema:

"Tulijua kwamba mamilioni ya nyoyo,vichwa na mikono ilikua nyuma ya wale waliouporomosha ukuta."

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amezungumzia jinsi mamilioni ya watu walivyokua sababu ya kuporomoka ukuta wa Berlin na sio wanasiasa.Na akawasiliasha pia risala kutoka kwa rais Barack Obama:

Kansela Angela Merkel ambae kabla ya hapo alitoa hotuba ya kusisimua,amewashukuru vivongozi wa kimataifa kwa kuunga mkono muungano.

"Mmedhihirisha imani yenu kwa nchi yetu.Kwasababu hiyo pia tunakushukuruni na tutaendelea kukushukuruni kwa dhati. "

Wakati huo huo katika eneo linalolizunguka bunge la Reichtag,maelefu ya watu walikua wakisubiri kuuona ukuta ukiporomoka.Matofali zaidi ya elfu moja ya sandarusi yaliyochorwa kwa rangi rangi na watoto 15 elfu yaliporomoka,moja baada ya jengine.Ukuta umeporomoka na hapo sherehe halisi zikaanza kati kati ya mji mkuu Berlin.

Mwandishi:Kiesel Heiner (DW Berlin)/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman