1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 10 leo tangu vita vya Kosovo

9 Juni 2009

Kosovo leo ni nchi huru ?

https://p.dw.com/p/I6PP

Leo, miaka 10 iliopita,vilimalizika vita vya Kosovo vilivyoongozwa na shirika la ulinzi la magharibi (NATO) na vilivyochukua muda wa siku 78. NATO ilishambulia vituo vya huko Serbia ,Kosovo kwenyewe na hata Montenegro.Shabaha ilikua kumlazimisha rais wa Serbia Slobodan Milosevic kuregeza kamba juu ya msimamo wake kuhusu Kosovo.

Miaka 10 baadae hii leo, Kosovo ingawa ni nchi huru rasmi, kimsingi lakini, inalindwa uhuru wake huu na jamii ya kimataifa.Kwani, hata wanajeshi wa Ujerumani wa Bundeswehr wanatumika huko bado katika kile kikosi cha KFOR.

Vita vya Serbia kupigana na NAT0 havikuwa na matumaini ya ushindi na wala havikuwa na faida yoyote kwake.Hivyo ndivyo alivyosema katibu wa dola wa wizara ya Serbia iliohusika na Kosovo,Oliver Ivanovic.

Rais wa zamani marehemu Slobodan Milosevic alianzisha vita dhidi ya dunia nzima ingawa tangu awali ilibainika dhahiri kuwa hangeshinda vita hivyo:

"Hakuna shaka yoyote ,vita vile tangu mwanzo ilijulikana Serbia haingeshinda.Kwavile ikipigana na dola 18 za NATO.Ilikuwa siasa za wazimu na msururu wa makosa kadhaa dhidi ya waalbania wa Kosovo na jirani zake.

Mwishoe,iliongoza kwa dunia nzima na hata washirika wetu wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya dunia kutugeukia."

Ilikuwa marehemu Milosevic na propaganda yake aliojidai kabla kutia saini mapatano ya "Kumanovo hapo Juni 9,1999 yaliokomesha vita hivyo vya siku 78 na kuhama kwa vikosi vya Serbia kutoka Kosvo eti ni ushindi mkubwa kwa Serbia.

Tangu Februari 17 mwaka jana Kosovo imekuwa nchi huru iliotambuliwa na mataifa 60 mbali mbali ulimwenguni.Miongoni mwa nchi hizo ni 22 zanachama wa Umoja wa Ulaya na hata Marekani .Mbali na serbia binafsi n a Bosnia-herzegovina,hata nchi zilizotokanana na kusambaratika kwa Shirikisho la yugoslavia,zimeitambua dola huru la Kosovo.

Kwa serikali ya Pristina, Kosovo ni nchi imara,ya kidemokrasi na ya usalama-asema waziri wa ndani wa kosovo Zenun Pajaziti:

"Kuwa Kosovo licha ya shida zake mbali mbali tulizokumbana nazo ni nchi tulivu,usalama wake umebakia tatizo la kisiasa.Hatahivyo, inatupasa kuendelea kujitahidi kupata imani ya wakaazi wake wa asili mbali mbalii.Taasisi za Kosovo zinatilia umuhimu mkubwa katika kutetea haki za jamii za wachache nchini.Kwa kuliungamkono Jeshi la KFOR la Umoja wa mataifa na EULEX-Tume ya sheria ya Umoja wa Ulaya,maendeleo yatafikiwa haraka na kwa nguvu zaidi."

Kwa jicho la Serbia,Kosovo miaka 10 tangu kumalizika vita "si nchi huru wala yenye usalama."

Kwa muujibu wa katibu wa dola wa Serbia anaehusika na swali la kosovo Ivanovic, huko Kosovo hakuna bado kabila moja lile la waserbia lenye matatizo mengi kwaku wa tu ni waserbia.tatizo liliopo ni hata kubwa zaidi: kwani Kosovo kuna maalfu ya wanajeshi wa kikosi cha KFOR na polisi wa kimataifa kinachowafanya waserbia kutohisi wako katika hali ya usalama."

Asema mserbia huyo.Hivi sasa kuna jeshi la askari 15.000 la KFOR huko Kosovo na kikosi cha askari 2.00 wa kimataifa na kiasi cha 8.000 wa kikosovo.

Mwanzoni mnwa mwaka huu kulianza mpango wa kuunda jeshi la ulinzi la wakosovo lenye askari 2.500 pamoja na wengine 800 askari wa akiba.Waziri wa ndani wa Kosovo adai lengo lake ni kuwafanya wakaazi wote wa Kosovo wanaishi kwa usalama.

Waziri wa ndani Pajaziti akaongeza kusema kwamba , kile ambacho hawawezi kuhakikisha ni usalama kwa wale watu waliohusika na uhalifu.Aliwataka waserbia kujiunga na taasisi za utawala wa Kosovo.

Waziri wa nje wa Ujerumani Frank walter Steinmeier amesem,a kuwa, Kosovo inakabiliwa na changamoto kubwa kujenga uchumi wake na kupambana na rushua na uhalifu ni sehemu tu ya changamoto hizo:

"Mvutano kati ya makabila mbali mbali imesalia katika balkan,muhimu zaidi ni kuwa shetani wa vita ameepukwa.Licha ya hatua zote ilizopiga Kosovo na eneo zima ,kuwapo majeshi ya kimataifa kutaendelea kuhitajika."

Alisema waziri wa nje wa Ujerumani.

Mwandishi:Cani Bahri/ZR/Ramadhan Ali

Mhariri:M.Abdul-Rahman