Mgongano baina ya unyago-asilia na unyago-mamboleo | Masuala ya Jamii | DW | 30.05.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mgongano baina ya unyago-asilia na unyago-mamboleo

Unyago, ambao kiasili ulifanyika kwa siri, ni mafunzo mazito ya ndani anayopewa mwanamke pale anapofikia umri wa kuweza kuolewa ili aweze kuidhibiti na kuilinda nyumba yake kama mke. Sasa 'siri' hii ya unyago haipo tena.

Watoto mjini Zanzibar

Watoto mjini Zanzibar

Unyago ni mila inayofanyika zaidi katika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki ikiwajumuisha watu wa makabila mbali mbali ya pwani ya eneo hilo.

Miongoni mwa mengine, lengo la mila hii ya asili ni kuimarisha jamii na kujenga uhusiano ulio bora zaidi kati ya mume na mke miongoni. Hata hivyo, kuja kwa mawasiliano ya kisasa ya mitandao, kumeanza kukiondoa kile kipengele muhimu cha usiri katika mila hii.

Hivi sasa, umaarufu wa unyago unaonekana kuchukuwa muelekeo mpya, baada ya mafunzo yake kuonekana kutawala katika blogu mbali mbali za kijamii. Katika makala hii ya Utamaduni na Sanaa, Saumu Mwasimba, anaangalia sio tu tofauti baina ya unyago-asilia na unyago-mamboleo unaofunzwa kupitia mitandao, bali pia faida na umuhimu wa mila hii.

Mwandishi/Mtayarishaji/Msimulizi: Saumu Mwasimba
Mhariri: Mohammed AbdulRahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 30.05.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11QsL
 • Tarehe 30.05.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11QsL

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com