Mgomo wa Wafungwa nchini Tanzania | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mgomo wa Wafungwa nchini Tanzania

Nchini Tanzania mgomo wa wafungwa sasa katika magereza mawili ya mjini Dar es Salaam, sasa umezagaa hadi mkoa wa kaskazini wa Arusha wakilalamika juu ya kuwekwa rumande muda mrefu bila ya kesi zao kukamilika. Baadhi ni wale walioko rumande kwa zaidi ya miaka 10 sasa.

Malalamiko yao yanafuatia kuachiwa kwa dhamana kwa kigogo mmoja nchini humo, anayekabiliwa na mashtaka ya kuuwa bila ya kukusudia. Saumu Mwasimba amezungumza na mtaalamu wa masuala ya sheria Profesa Isa Shivji na kwanza alimuuliza wanaionaje hali hii ya watu wa rumande muda mrefu bila ya kesi kukamilishwa pamoja na msongamano wa wafungwa magerezani.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com