1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea urais wa Chama cha Wananchi, CUF, Seif Sharif Hamad atangaza sera na nadharia yake

17 Agosti 2010

Joto la kisiasa lazidi Zanzibar huku uchaguzi wa Oktoba 31 ukikaribia nchini Tanzania

https://p.dw.com/p/OpHS
Seif Sharif HamadPicha: DW

Visiwani Zanzibar joto la uchaguzi linazidi kupamba moto na wagombea wa urais wa vyama tofauti tayari wameshachukua fomu za kuwania wadhifa huo. Zoezi hilo lilianza jana Jumatatu. Kwa sasa ni vyama vitatu vilivyowasilisha wagombea wake vya Chama cha Wananchi,CUF, Chama cha NCCR-Mageuzi na Chama cha Wakulima cha AFP. Mwakilishi wa Chama cha Sauti ya Umma, SAU, alinyimwa fomu baada ya wagombea wawili kujitokeza wakitaka kuiwania nafasi hiyo kinyume na taratibu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, ZEC.

Pindi baada ya kuchukua fomu, wagombea hao walizitangaza sera na nadharia zao. Mgombea wa urais wa Chama cha Wananchi,CUF, Seif Sharif Hamad alisisitiza kuwa jambo la muhimu ni kuyaimarisha maisha ya Wazanzibari wa kawaida. Mwandishi wetu wa Visiwani Zanzibar Salma Said alipata nafasi ya kufanya mahojiano maalum na mgombea huyo wa CUF anayeanza na kuielezea nadharia yake.