1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfumko wa bei washuka nchini Tanzania

17 Machi 2010

Taasisi ya Takwimu ya Taifa nchini Tanzania-NBS, imetoa takwimu zinazoonyesha kuwa mfumko wa bei umepungua kwa asilimia 9.6 kwa mwezi uliopita wa Februari.

https://p.dw.com/p/MUXH

 Hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwezi Agosti, mwaka 2008 na kwamba serikali ina uhakika utaendelea kupungua katika miezi michache ijayo. Hata hivyo baadhi ya wachumi wana wasi wasi kama kweli hatua hiyo itafanikiwa kutokana na uvunaji mdogo wa mazao. Grace Kabogo alizungumza na Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzani-BoT, Geoffrey Mwambe na alianza kwa kuelezea hasa kuhusu kushuka kwa kiwango hicho cha mfumko wa bei.

Mtayarishi: Grace Kabogo

Mhariri:M.Abdul-Rahman